Loading...

TANESCO yaanza rasmi operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali.

Shirika la umeme nchini TANESCO limeanza operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli alilotoa hivi karibuni.

Kaimu meneja uhusiano wa TANESCO Bi Leila Muhaji amesema zoezi hilo limeanza nchi nzima na kuongeza kuwa shirika hilo lilitoa muda wa siku kumi na nne wadaiwa wawe wamelipa madeni yao lakini hadi leo wapo ambao bado wako kimya.

Baadhi ya wananchi wamekuwa wamekuwa na maoni tofauti juu ya suala hilo huku wengine wakiishauri tANESCO kufungia taasisi za serikali luku ili waweze kulipa kadiri wanavyotumia.

Licha ya uwepo wa madeni hayo ambayo TANESCO inadai yanasababisha wajiendeshe kwa hasara, taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali iliyokabidhiwa kwa rais inaeleza kuwa shirika hilo linajiendesha kwa hasara ambapo linanunua umeme shilingi 544 kwa unit lakini inauza kwa shilingi 279 kwa unit.

Source:ITV
TANESCO yaanza rasmi operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali. TANESCO yaanza rasmi operesheni ya kuwakatia umeme wadaiwa sugu zikiwemo taasisi za serikali. Reviewed by Zero Degree on 3/28/2017 08:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.