Loading...

Zaidi ya vijana 4,800 wameathirika na dawa za kulevya wilayani Ilemela.

Zaidi ya vijana 4,800 katika wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza wamegundulika kuathirika na dawa za kulevya, huku vijana 150 wilayani humo,wakiwemo 22 wa kata moja tu ya kirumba wakiripotiwa kupoteza maisha,jambo linalofanya mkoa wa Mwanza kushika nafasi ya pili kitaifa katika matumizi ya dawa za kulevya baada ya mkoa wa Dar es Salaam.

Ushuhuda huo umetolewa jijini Mwanza na Mratibu wa taasisi ya Chinga Respect Complex Denis Nyamlekela ambaye taasisi yake inayoshirikiana na Ofisi ya Waziri mkuu kupitia Wizara ya kazi, vijana, ajira na walemavu anasema kata ya Kirumba ndiyo kitovu cha dawa za kulevya katika mkoa wa Mwanza.

Elisha Majukano ni mkazi wa Kirumba jijini Mwanza amejitokeza kutoa ushuhuda wa namna alivyoanza kutumia madawa ya kulevya tangu akiwa shule ya msingi hadi alipojiunga na Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda,huku baadhi ya vijana wengine waliokuwa watumiaji wa dawa za kulevya wakisimulia walivyoathirika

Dk. Jacob Mutashi, Afisa usalama wa taifa mstaafu mkoa wa Mwanza anasema kiafya dawa za kulevya zinasababisha magonjwa ya akili,mapafu,moyo,ini na figo na hata kusababisha vifo vya ghafla hasa miongoni mwa vijana wanaojidunga kutokana na kuzidisha dozi.

Hapa mkoani mwanza zao la bangi hulimwa kwa wingi katika wilaya ya sengerema kutokana na uwepo wa misitu ya hifadhi na pia dawa hizo huingizwa jijini hapa kwa njia ya mabasi kutokea wilaya ya tarime mkoani mara,tabora na simiyu na kwa kutumia usafiri wa mitumbwi ndani ya ziwa victoria.

Source: ITV
Zaidi ya vijana 4,800 wameathirika na dawa za kulevya wilayani Ilemela. Zaidi ya vijana 4,800 wameathirika na dawa za kulevya wilayani Ilemela. Reviewed by Zero Degree on 3/14/2017 01:06:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.