Loading...

Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha zake za nusu utupu kuzua gumzo

Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha yake inayomuonyesha akiwa utupu kusababisha maneno mengi mitandaoni.

Muimbaji huyo amerudi tena kupitia mtandao wa Instagram kwa kuweka video ambayo inamuonyesha akiwa mtupu huku ukisikika wimbo ukiimba na kuandika, “Usi-judge kitabu kama hujakisoma ndani.”



Hata hivyo imeonyesha kuwa picha hizo zilizozua utata mkubwa mapema wiki hii ni ujio wa nyimbo yake mpya ya Ben ambayo imedaiwa kupewa jina la ‘Mateka’ na ndani yake amemshirikisha rapper Darassa.

Wimbo huo pia umetayarishwa na Tiddy Hotter ambaye alitengeneza wimbo mwingine wa Phone wa Ben.
Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha zake za nusu utupu kuzua gumzo Ben Pol amefunguka kwa mara ya kwanza tangu picha zake za nusu utupu kuzua gumzo Reviewed by Zero Degree on 5/21/2017 05:49:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.