Loading...

Liverpool yatupwa nje ya michuano ya Kombe la EFL [Carabao]


Islam Slimani alifunga bao kwa kombora kali na kuwasaidia Leicester kuwalaza Liverpool 2-0 katika mechi ya raundi ya tatu ya Kombe la Carabao, ambao pia hufahamika kama Kombe la EFL, uwanjani King Power Jumanne.



Mchezaji huyo wa Algeria alifunga kwa mguu wa kushoto baada ya nguvu mpya Shinji Okazaki kuwaweka Leicester kifua mbele.

Mabao hayo yalipatikana baada ya Liverpool kutawala kipindi cha kwanza ambapo Philippe Coutinho alikuwa amecheza vyema sana kabla ya kuondolewa uwanjani.

Okazaki aliingia uwanjani na kuwaongezea nguvu Leicester na kufunga kutoka kwa pasi safi iliyotoka kwa Vicente Iborra.

Alex Oxlade-Chamberlain na Dominic Solanke walionunuliwa na Liverpool majuzi wote walipoteza nafasi nzuri za kufunga.

Kwingineko Roy Hodgson alipata ushindi wake wa kwanza Crystal Palace wakiwa nyumbani dhidi ya Huddersfield.

Bristol City nao waliwashangaza Stoke City.

Tottenham nao walichukua dakika 65 kuwapangua Barnsley uwanjani Wembley nao Leeds wakawalaza Burnley kwa mikwaju ya penalti uwanjani Turf Moor.


Liverpool watasafiri tena Leicester kwa mechi ya Ligi ya Premia siku ya Jumamosi, mechi ambayo itaanza saa moja unusu jioni saa za Afrika Mashariki.
Matokeo kamili ya mechi za Jumanne
  • Crystal Palace 1-0 Huddersfield Town
  • Aston Villa 0-2 Middlesbrough
  • Brentford 1-3 Norwich City
  • Bristol City 2-0 Stoke City
  • Burnley 2-2 Leeds United (Leeds wakashinda kwa penalty 5-3)
  • AFC Bournemouth 1-0 Brighton & Hove Albion
  • Leicester City 2-0 Liverpool
  • West Ham United 3-0 Bolton Wanderers
  • Wolverhampton Wanderers 1-0 Bristol Rovers
  • Reading 0-2 Swansea City
  • Tottenham Hotspur 1-0 Barnsley
Liverpool yatupwa nje ya michuano ya Kombe la EFL [Carabao] Liverpool yatupwa nje ya michuano ya Kombe la EFL [Carabao] Reviewed by Zero Degree on 9/20/2017 10:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.