Myanmar: Aung San Su Kyi akosolewa na Viongozi wa dunia
Wakati wa hotuba yake ya siku ya Jumanne, kiogngozi huyo alilaani ukiukaji wa haki za binadamu lakini hakulaumu jeshi au kuzungumzia madai yanayohusu mauaji wa kikabila.
Viongozi na wanadiplomasia wa nchi kadha tangu wameelezea kughadhabishwa kwao na msimamo wake Suu Kyi.
Zaidi ya watu 400,000 wa Rohinya wamekimbia kwenda Bangladesh tangu mwezi Agosti.
Zaidi ya watu 400,000 wa Rohinya wamekimbia kwenda Bangladesh tangu mwezi Agosti.
Mzozo wa hivi majuzi katika jimbo la Rakhine ulianza baada ya mashambulizi katika vituo vya polisi kote katika jimbo hilo mwezi uliopita, yanayolaumiwa kwa kundi ambalo limeibuka la Arakan Rohingya Salvation Army (Arsa).
Watu kadha waliuawa wakati wa operesheni iiyoendeshwa na jeshi na kuna madai mengi kuwa vijiji vinachomwa moto na watu wa Rohinya kulazimishwa kuhama.
Watu kadha waliuawa wakati wa operesheni iiyoendeshwa na jeshi na kuna madai mengi kuwa vijiji vinachomwa moto na watu wa Rohinya kulazimishwa kuhama.
Rahingya ni jamii ya waislamu ambayo imenyimwa uraia na serikali ya Myanmar inayosema kuwa wao ni wahamiaji haramu kutoka Bangladesh.
Myanmar: Aung San Su Kyi akosolewa na Viongozi wa dunia
Reviewed by Zero Degree
on
9/20/2017 12:00:00 PM
Rating: