Yaliyotokea nje ya uwanja baada ya Neymar na Cavani kugombea penati
Nyota wa Paris Saint-Germain, Neymar ameripotiwa kuacha kufuata (Unfollow) ukurasa wa mchezaji mwenzake, Edinson Cavani Instagram.
Wawili hao walitofautiana wikendi iliyopita, wakati Neymar alipoung'anga'ania mpira ikiwa Cavani alikuwa tayari anauandaa kwa ajili ya kupiga mpira wa adhabu walipocheza dhidi ya Lyon.
Nyota huyo aliyevunja rekodi kwa kusajiliwa kwa pesa nyingi zaidi alijaribu kufanya kitu sawa na kile alichofanya Cavani aliposogea mbele kujaribu kupiga penati.
Lakini raia huyo wa Uruguay alikataa kumuachia Neymar penati hiyo kabla hajashuhudia shuti lake likiokolewa na mlinda mlango wa timu pinzani.
Mbrazili mwenzake, Dani Alves pia alionekana akijaribu kumtetea Neymar ili apewe nafasi ya kupiga penati kwa kumzuia Cavani.
Na mtandao wa 'Get French Football' unadai kwamba, Cavani alionyesha kuchukizwa na kitendo hicho mwishoni mwa mchezo.
Inasemekana kwamba, dakika 20 baada ya kipenga cha mwisho, Cavani alikuwa tayari amekwisha panga mizigo yake na kuondoka.
Pia aliamua kuacha kupita sehemu zenye mchanganyiko wa watu pamoja na wachezaji wenzake kwa kuondoka uwanjai hapo kupitia mlango wa nyuma.
Na sasa Neymar amejibu mapigo hayo kwa kumundoa Cavani kwenye orodha ya watu anaowafuatilia kwenye mitandao ya kijamii, kitu ambacho kinaonekana kuwa chanzo cha mgogoro ndani ya klabu hiyo.
Hata hivyo, inaonyesha kwamba kocha wa klabu jiyo, Unai Emery anahisi kila kitu kipo chini ya uangalizi na hatarajii kuingilia suala hilo.

Alisema: “Nimewaambia watafute suluhisho la tatizo hilo wao wenyewe."
Yaliyotokea nje ya uwanja baada ya Neymar na Cavani kugombea penati
Reviewed by Zero Degree
on
9/19/2017 10:49:00 AM
Rating: