Loading...

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari atumbuliwa

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza.
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemuagiza Katibu mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe kumsimamisha kazi mara moja Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Ndg Henry J. Semwanza kuanzia leo Novemba 9, 2017.

Waziri wa kilimo, Mhe. Dkt. Charles Tizeba
Kwa agizo hilo lililotolewa na Waziri wa Kilimo Dkt Tizeba, Mkurugenzi huyo atatakiwa kurejea kwa mwajiri wake ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kupangiwa kazi nyingine.

Semwanza anasimamishwa kazi kutokana na mwenendo wake wa utendaji akiwa Msimamizi Mkuu wa Bodi ya Sukari kutoridhisha.

Semwanza amehudumu katika nafasi hiyo akiwa Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari tangu mwaka 2011.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari atumbuliwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari atumbuliwa Reviewed by Zero Degree on 11/10/2017 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.