Loading...

Droo kamili ya Ligi ya Europa hatua ya 32 bora


Arsenal imepangwa kucheza dhidi ya timu ya Ostersunds ya nchini Sweden katika Hatua ya 32 Bora ya michuano ya Europa League.

Arsenal itawavaa wapinzani wao hao ambao wanafundishwa na Graham Potter ambaye ni raia wa Uingereza.

Atletico Madrid wao wamepangwa kukutana na Copenhagen wakati Borussia Dortmund itakutana na wabishi kutoka Italia, Atalanta ambao waliifunga Everton nyumbani na ugenini katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Makocha wawili waliowahi kufanya kazi England wanatarajia kukutana pia katika hatua hiyo wakati ambapo Celtic inayonolewa na Brendan Rodgers itakutana na Zenit St Petersburg iliyochini ya Roberto Mancini.

Kocha Gennaro Gattuso wa AC Milan ataiongoza timu yake hiyo kuivaaa Ludugorets ya Bulgaria.

Ratiba kamili inaonyesha hatua hiyo itachezwa Februari 15 wakati mechi za marudio ni Februari 22, mwakani 2018.

Droo Kamili ya Ligi ya EUROPA: 

  • Borussia Dortmund vs Atalanta
  • Nice vs Lokomotiv Moscow
  • Copenhagen vs Atletico Madrid
  • Spartak Moscow vs Athletic Bilbao
  • AEK Athens vs Dynamo Kiev
  • Celtic vs Zenit St Petersburg
  • Napoli vs Leipzig
  • Red Star Belgrade vs CSKA Moscow
  • Lyon vs Villarreal
  • Real Sociedad vs Salzbug
  • Partizan Belgrade vs Viktoria Plzen
  • Steaua Bucharest vs Lazio
  • Ludogorets vs AC Milan
  • Astana vs Sporting Lisbon
  • Ostersunds vs Arsenal
  • Marseille vs Braga
Droo kamili ya Ligi ya Europa hatua ya 32 bora Droo kamili ya Ligi ya Europa hatua ya 32 bora Reviewed by Zero Degree on 12/11/2017 04:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.