Loading...

Nyalandu atuma salamu za pole kwa Rais Magufuli


ALIYEKUWA Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, jana Disemba 11, 2017 alituma salamu za pole kwa Rais na Amri Jeshi Mkuu, Dkt. John Pombe Magufuli kufuatia vifo vya askari 14 wa JWTZ waliouawa nchini DR Congo walikokuwa wakilinda amani.

Miili ya askari hao ikiwasilii Tanzania
Nyalandu alitumia ukurasa wake wa Facebook kutuma salamu zake za pole kwa Rais Magufuli na familia za askari hao waliouwawa na wale waliojeruhiwa katika mapigano makali yaliyotokea nchini humo Disemba 7 na 8 kati ya askari wa Tanzania na Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) yaliyopelekea askari hao 14 wa Tanzania kupoteza maisha huku wengine 44 wakiwa wamejeruhiwa na wawili wengine kutojulikana walipo.

“Natoa pole kwa Mhe. Rais Magufuli na wanafamilia wote kufuatia kuuawa kwa maaskari 14 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)” alindika Nyalandu.

Ujumbe wa Nyalandu
Miili ya wanajeshi hao iliwasili jijini Dar es Salaam jana kwa ndege maalum ya Umoja wa Mataifa, ambapo ilipelekwa kwenye Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi ambapo Desemba 14 itaagwa.

Taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Augustine Mahiga akihojiwa na moja ya vituo vya redio alisema askari wote waliokuwa hawaonekani wamepatikana na uchunguzi unaendelea kwani inaonyesha mmoja wao kama alikuwa ameshikiliwa mateka.
Nyalandu atuma salamu za pole kwa Rais Magufuli Nyalandu atuma salamu za pole kwa Rais Magufuli Reviewed by Zero Degree on 12/12/2017 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.