Loading...

Oscar Pistorius apata majeraha katika mkono wake baada kupigana gerezani

Oscar Pistorius (kushoto) akielekea mahakamani mwaka 2016
Mwanariadha wa zamani wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ameumizwa mkono wake wakati akipigana gerezani wiki chache baada ya kesi ya kumuua aliyekuwa mchumba wake Reeva Steenkamp kusikilizwa tena.

Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, msemaji wa gereza hilo alisema mwanariadha huyo mlemavu aliyefungwa miaka 13 alihusika kati ugomvi wa kugombea simu ya umma uliomsababishia akwaruzike ngozi yake ya mkono. Hakuna majeraha mengine yaliyotajwa kumpata mwanariadha huyo.

Tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 7, siku kumi baada ya waendesha mashitaka wa Afrika Kusini kukubali adhabu ya kifungo cha miaka sita kilichokuwa kikimkabili Pistorius kuongezwa na kuwa miaka 13.
Oscar Pistorius apata majeraha katika mkono wake baada kupigana gerezani Oscar Pistorius apata majeraha katika mkono wake baada kupigana gerezani Reviewed by Zero Degree on 12/13/2017 12:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.