Loading...

Wizara ya Nishati yatakiwa kujiridhisha na ubora wa vifaa katika miradi ya umeme


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati ijiridhishe na ubora wa vifaa vinavyotumiwa na wakandarasi katika miradi ya umeme.

Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza katika kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika , Ofisini kwake, Dodoma ambapo ametaka iwasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya miradi inayotekelezwa inalingana na kiasi cha fedha wanacholipwa wakandarasi hao.

Waziri Mkuu amesema wakati huu ambao Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakiendelea na miradi ya usambazaji umeme, na kuongeza kwamba ni vema wizara hiyo ikajiridhisha na ubora wa vifaa.

“Wasimamieni wakandarasi kikamilifu na kama hamjaridhishwa na kazi wanayofanya msisite kuwachukulia hatua, tunataka wananchi wapate umeme.” Majaliwa

Amesema Rais Dkt. John Magufuli amedhamiria kuona umeme unasambazwa kwenye vijiji vyote nchini kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.

Waziri Mkuu amesisiza kwamba ni lazima wakandarasi waliopewa jukumu hilo wasimamiwe kikamilifu ili mradi hiyo iweze kuwa na ubora unaostahili.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema tayari wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA namba tatu wameshaanza kazi.

Amesema kwa wakandarasi ambao bado hawajaanza wamekubaliana kwamba wataanza wakati wowote na wa mwisho utaanza Machi 2, 2018 na kuongeza kwamba wizara yake itahakikisha miradi yote ya kusambaza umeme inasimamiwa kikamilifu na inakamilika kwa wakati na katika ubora unaostahili.
Wizara ya Nishati yatakiwa kujiridhisha na ubora wa vifaa katika miradi ya umeme Wizara ya Nishati yatakiwa kujiridhisha na ubora wa vifaa katika miradi ya umeme Reviewed by Zero Degree on 1/13/2018 08:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.