Loading...

Atletico Madrid inataka wachezaji wawili kutoka Liverpool


Atletico Madrid inatarajiwa kufanya mabadiliko makubwa kwenye usajili wa majira ya joto. Vigogo hao wa Uhispania wanakabiliwa na hofu ya kumpoteza Antoine Griezmann na Jan Oblak lakini wanaweza kuwatumia nyota hao kwa faida ya kukijenga upya kikosi chao, kwa mujibu wa Don Balon.
Griezmann anaweza kujiunga na klabu ya Barcelona kwenye majira ya joto. Wakati vinara hao wa La Liga wakiwa tayari kulipa kiasi kinachohitajika kumnasa Mfaransa huyo, Diego Simeone bado ana matumaini kuwa nyota huyo atasalia katika klabu hiyo hadi msimu ujao. Golikipa wao, Jan Oblak pia amekuwa akihusishwa na klabu kubwa za Ulaya ikiwemo Paris Saint-Germain.

Ripoti zanadai kuwa Simeone ana mipango mikubwa kwa kikosi chake kwenye usajili wa majira ya joto, ikiwa ni pamoja na kujaza nafasi zitakazoachwa wazi na nyota watakaoondoka kikosini. Atatumia fedha atakazopata kusajili wachezaji wapya kwenye majira ya joto.
Kwa mujibu wa ripoti hizo, meneja huyo anatamani kuwasajili wachezaji wawili wa Liverpool, Sadio Mane na Emre Can. Ingawa Salah ameteka vichwa vingi vya habari magazetini, Mane amekuwa mchezaji wa muhimu pia, akionyesha uwezo wake na thamani yake msimu huu. Amekuwa mchezaji muhumi kwa timu tangu aliposajiliwa na Jurgen Klopp mwaka 2016.

Emre Can anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto, huku mkataba wake ukitarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu. Juventus tayari imeshampa ofa lakibi kiungo huyo bado hajatoa jibu lolote.
Wote Mane na Can ni aina ya wachezaji wanaojituma sana ambao Simeone anapendelea, na ni rahisi kufukiri kwamba watakuwa na mafanikio makubwa kwenye La Liga.

Hili linaweza kuwa pigo kubwa kwa Liverpool, huku mfungaji bora wa klabu hiyo Salah tayari anahusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid na Barcelona na hawawezi kuwa tayari kuwapoteza nyota wao kwa mpigo kwenye dirisha moja la usajili.
Atletico Madrid inataka wachezaji wawili kutoka Liverpool Atletico Madrid inataka wachezaji wawili kutoka Liverpool Reviewed by Zero Degree on 4/24/2018 07:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.