Loading...

Guardiola anaamini huyu ndiye anayefaa kuchua nafasi ya Wenger

Pep Guardiola
Arsene Wenger alitangaza siku ya Ijumaa kuwa ataondoka Arsenal mwishoni mwa msimu ujao baada kuiongoza klabu hiyo kwa miaka 22. The Gunners wanatarajiwa kuanza mchakato wa kusaka mrithi wa Mfaransa huyo.
Moja wa wagombea wa nafasi huyo ni Patrick Viera. Alikuwa nahodha wa Arsenal wakati klabu hiyo ilipokuwa na kiwango cha hali ya juu sana chini ya Wenger mwanzoni mwa karne hii, akifanikiwa kuitawala safu ya kiungo wakati klabu hiyo ilipoibuka kidedea msimu wa 2003-04.

Kwa sasa ni mkufunzi mkuu wa New York City, ambayo iko chini ya kivuli cha Manchester City. Pep Guardiola anahisi ameshuhudia uwezo wake vya kutosha katika miaka yake miwili akiwa na Manchester City kiasi cha kusema kwamba Vieira anaweza kuikabili changamoto hiyo na yuko tayari kuchukua nafasi ya Wenger kama meneja mpya wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Goal, meneja huyo wa Manchester City alipoulizwa kama Vieira anaweza kuwa meneja katika ngazi za juu alisema: “Bila shaka, yuko tayari”.

“Sasa, kufuatia kilichotokea [tangazo la Wenger] kutakuwa majina mengi yatakayohusishwa.

“Naamini Arsenal inaenda kufanya uamuzi bora katika hilo. Lakini hata yeye yuko tayari kwa kazi hiyo.

“Nafikiri majina yote yatakayoanza kutajwa yatakuwa tayari kwa kazi hiyo.”
Guardiola anaamini huyu ndiye anayefaa kuchua nafasi ya Wenger Guardiola anaamini huyu ndiye anayefaa kuchua nafasi ya Wenger Reviewed by Zero Degree on 4/23/2018 11:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.