Loading...

Je, Manchester United itakamilisha usajili wa kiungo huyu mapema kabla ya Real Madrid?

Leandro Paredes
Manchester United wana mpango wa kumsajili aliyekuwa kiungo wa klabu ya Roma, Leandro Paredes lakini wanaweza kukumbana na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Real Madrid.
Klabu nyingi zitahitaji kumaliza mipango yao ya usajili mapema iwezekanavyo kwenye majira ya joto, lakini haitokuwa rahisi kwa vigogo ambao wanatamani kuipata saini ya kiungo wa klabu ya Zenit St Petersburg, ‘Leandro Paredes’.

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Argentina ameshasema kuwa hatafanya uamuzi wowote kuhusiana na hatima yake hadi baada ya Kombe la Dunia.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka nchini Italia, mahasimu wa Man United’, Liverpool walitoa ofa ya pauni milioni 26.5 kwa ajili ya Paredes mwezi January 2017, na tangu hapo amekuwa akizivutia klabu za Real Madrid na Juventus.

Paredes amekuwa tegemezi kwenye kikosi cha Jorge Sampaoli cha Argentina. Muda wa michuano ya Kombe la Dunia utakapowasili, Mascherano na Biglia wote watakuwa na umri wa miaka 33, hivyo Paredes anaweza kupewa kibarua muhimu kwenye timu ya taifa.

Kama Paredes ataonyesha uwezo mkubwa kwenye Kombe la Dunia, thamani yake inaweza kuongezeka hadi kufikia kati ya pauni milioni 50 na 60.
Je, Manchester United itakamilisha usajili wa kiungo huyu mapema kabla ya Real Madrid? Je, Manchester United itakamilisha usajili wa kiungo huyu mapema kabla ya Real Madrid? Reviewed by Zero Degree on 4/17/2018 11:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.