Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 19 Aprili, 2018

Antoine Griezmann na Diego Simeone
Mkufunzi wa Atletico Madrid, Diego Simeone anaamni mshambuliaji wa klabu hiyo, Antoine Griezmann anaweza kushawishika kubaki kama klabu hiyo ya Uhispania itafanikiwa kuifunga Arsenal kwenye Europa Ligi. (AS)

Arsene Wenger anasema kuwa Santi Carzola anaweza kupewa ofa ya mkataba mpya, ingawa Mhispania huyo anakabiliana na kuokoa hatima yake kisoka baada ya kuwa nje tangu mwezi Octoba mwaka 2016. 

West Ham inatarajiwa kumpa mkataba mpya David Moyes na inaweza kuwa tayari kumpa madaraka yote ya kuiongoza klabu hiyo. (Evenin Standard)

Andrea Belotti anaweza kusalia katika Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa mwaka mwingine, huku klabu ya Torino ikiwa na nia ya kuendelea kumng'ang'ania mshambuliaji huyo. (Tuttosport)
 
Clement Lenglet mepiga hatua moja mbele kukaribia kufikia makubaliano na klabu ya Barcelona baada ya mawakala wake na wale wa klabu hiyo kukutana wiki hii.

Barcelona wako kwenye mazungumzo na Samuel Umtiti juu ya kandarasi mpya, huku vinara hao wa La Liga wakitazamia kufikia makubaliano na Mfaransa huyo kabla ya Kombe la Dunia. (Sport)

Meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson anasema kuwa anataka kumbakisha Wilfried Zaha na nyota huyo hafikirii kuondoko katika klabu hiyo kwenye majira ya joto.
  
Beki wa Crystal Palace, Aaron Wan-Bissaka amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Uingereza utakaoisha mwaka 2020.

Alvaro Morata
Juventus inaweza kuwa na wakati mgumu kumrejesha Paul Pogba au Alvaro Morata kama watawekwa sokoni kwenye majira ya joto, kwa mujibu wa Giusepe Marotta.

Henrikh Mkhitaryan anaweza kurejea kutoka majreruhi kwenye mechi ya Europa Ligi kati ya Arsenal na Atletico Madrid Alhamisi

Arsene Wenger amesema kuwa hana uhakika kama Jack Wilshere anataka kusaini kandarasi mpya katika klabu ya Arsenal.

Harry Cochrane amesaini mkataba mpya katika klabu ya Hearts, baada ya kuwa na mafanikio msimu huu.

Beki wa klabu ya Chelsea, Marcos Alonso amepigwa marufuku ya michezo mitatu baada ya kumchezea vibaya Shane Long wa Southampton.

Andreas Pereira amethibitisha kwamba, klabu ya Valencia imemwambia wakala wake kuwa inataka kumsajili. (Sky Sports)

Hatima ya Paul Pogba Manchester United iko shakani, Jose Mourinho akipanga kuitibulia Manchester City na kumsajili kiunga anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50, Fred kutoka Shakhtar Donetsk.

Ruben Neves
Aliyekuwa meneja wa Bournemouth, Harry Redknapp amemshauri Lewis Cook kukataa ofa kutoka Manchester United.

Wolves wako tayari kupeleka ofa Arsenal kwa ajili ya usajili wa kiungo wa klabu hiyo, Jack Wilshere kwenye majira ya joto.

Chelsea wanatarajiwa kuomba kiasi cha pauni milioni 50 kwa ajili ya Michy Batshuayi, huku klabu ya Borussia Dortmund ikiwa na nia ya kumsajili rai huyo wa Ubelgiji moja kwa moja.

Layvin Kurzawa anawaniwa na Chelsea, Tottenham na Manchester United baada ya beki huyo wa kushoto kuambiwa kuwa anaweza kuondoka PSG, ambao wanalengo la kuongeza fedha kukidhi vigezo vya FFP. (Mirror)

Chelsea wana nia ya kumpa kibarua meneja wa klabu ya Napoli, Maurizio Sarri na achukue nafasi ya Antonio Conte. (Star)

Everton wanatafakari juu ya kupeleka ofa mpya kwa ajili ya winga wa klabu ya Porto, Yacine Brahimi kwenye majira ya joto baada ya ofa yao ya pauni milioni 35 kukataliwa mwaka jana.

Arsenal wanatazamia kumsajili beki wa klabu ya Fulham, Ryan Fredericks, ambaye atakuwa mchezaji huru kwenye majira ya joto.

Luke Shaw
Manchester United watahitaji angalau pauni milioni 28 kwa ajili ya Luke Shaw kama watamuuza kwenye majira ya joto kufuatia kutofautiana na mkufunzi wa klabu hiyo, Jose Mourinho. (Sun)

Mshambuliaji wa klabu ya Celtic, Moussa Dembele anawindwa na klabu ya Villarreal, ambayo inapanga kupeleka ofa ya pauni milioni 15 baada ya kupata pauni milioni 35 kwa kumuuza Cedric Bakambu kwenda Beijing Guoan mwezi Januari. (Express)

Patrick Vieira anapewa nafasi kubwa kuweza kuchukua nafasi ya Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal, ambaye anaweza kuondoka mwishoni mwa msimu huu.

Wolves wana mpango wa kushtukiza usajili wa kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere baada ya kujihakikishia nafasi ya kupanda daraja kushiriki Ligi Kuu ya Uingereza.

Crystal Palace wanaweza kumuuza Christian Benteke kwenye majira ya joto baada ya mkufunzi wa klabu hiyo, Roy Hodgson kuchoshwa na ukame wa magoli kutoka kwa straika huyo.

Marouane Fellaini anatarajiwa kuondoka Manchester United kwenye majira ya joto na kufuata pesa nyingi, huku klabu za China na MLS zikihusishwa na nyota huyo. (Daily Mail)

Roman Abramovich anashauriwa kufanya mabadiliko na kuteua meneja mwenye umri mdogo kama mbadala wa Antonio Conte, badala ya kuteua jina kubwa na maarufu.

Kumetokea mgawanyiko kati ya vigogo wa klabu ya Arsenal juu ya nani anafaa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger, ambaye anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)

Kieran Tierney
Kieran Tierney anasema kuwa kinachomvutia ni kuendelea kushinda mataji mengi akiwa na Celtic, licha ya kuhusishwa na uhamisho kwenda Manchester United. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 19 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 19 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/19/2018 11:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.