Loading...

Breaking News: ACT Wazalendo na CHADEMA waungana


Vyama vya upinzani ACT Wazalendo na CHADEMA vimeafikiana kuweka mgombea mmoja wa Ubunge anayekubalika katika jimbo la Buyungu ili kurudisha jimbo hilo mikononi mwa upinzani.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amesema kuwa makubaliano hayo yameafikiwa pia na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe ambapo kwa pamoja wataangalia mgombea mwenye ushawishi zaidi katika jimbo hilo iwe kutoka ACT Wazalendo au CHADEMA na kumuweka kuwa mgombea rasmi wa ubunge.

“Kwa heshima ya Mwalimu Bilago Mimi na Freeman Aikaeli Mbowe tumekubaliana kuwa tutashawishi kuwepo na a Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu. Ama Act Wazalendo itaunga mkono mgombea wa CHADEMA au CHADEMA itaunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo. Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na Wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi,amesema Zitto Kabwe na kueleza lengo la kufanya hivyo.

“Huu ni mwanzo wa harakati za kuwa na United Democratic Front dhidi ukandamizaji wa Demokrasia nchini na dhidi ya Hali mbaya ya Maisha ya Watu wetu. Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Wakulima, Vyama vya Wafanyabiashara na Wananchi wengine." amemaliza Zitto.

Jimbo la Buyungu kwa sasa lipo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA, Kasuku Samson Bilago kufariki dunia mnamo Mei 25, 2018 .
Breaking News: ACT Wazalendo na CHADEMA waungana Breaking News: ACT Wazalendo na CHADEMA waungana Reviewed by Zero Degree on 5/30/2018 06:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.