Kenya kurusha Setelaiti yake ya kwanza Ijumaa hii
Waziri wa Elimu wa Kenya, Amina Mohamed, ataongoza ujumbe utakaoshuhudia tukio hilo. Satelaiti hiyo ya mraba yenye ukubwa wa 10-kwa-10-kwa-10, itakuwa na faida kadhaa kwa Kenya ukiwemo utabiri wa hali ya hewa, uchoraji wa ramani, uchunguzi wa mazingira na wanyama.
Pia itatumika katika kuisaidia sekta ya vyombo vya habari nchini humo. Faida nyingine ni kusaidia usimamizi na uchunguzi wa mazingira ya anga za juu na majanga mbalimbali. Profesa/Mhandisi wa Chuo Kikuu cha Nairobi, amesema satelaiti hiyo ina uzito wa kilo 1.2 na na itakuwa juu umbali wa kilomita 4,000 kutoka duniani.
“Satelaiti za Nano hivi sasa ni vyombo vipya vinavyotumika katika utafiti wa anga za juu na shughuli za kibiashara. Ni teknolojia mpya itakayofanyiza jukumu kubwa la uchunguzi wa baadaye kwa kutumia satelaiti,” anasema Prof. Mbuthia. Chombo hicho kimetengenezwa kwa gharama ipatayo Ksh. Milioni 100 (sawa na Tsh. 22.78 bilioni) na kitadumu kwa kati ya miezi 12 hadi 18.
Kenya kurusha Setelaiti yake ya kwanza Ijumaa hii
Reviewed by Zero Degree
on
5/08/2018 06:25:00 PM
Rating: