Loading...

Maalim Seif ampatia majukumu Dkt. Bashiru


Chama cha Wananchi CUF, pamoja na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif amempongeza Katibu Mkuu mpya wa CCM, Dkt. Bashiru Ally ambapo pia wamempatia jukumu la kuirejesha demokrasia nchini.

Kupitia taarifa hiyo ya CUF Maalim Seif amesema Lazima malsahi ya Taifa la Tanzania yawe juu ya mipaka ya vyama vya siasa.

"Napenda kuchukua fursa hii adhimu kukupongeza Ndugu Dkt. Bashiru Ally kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM . Ni matarajio ya CUF na Watanzania kwa ujumla kuwa kwa nafasi hiyo kubwa ndani ya Chama chako utaitumia vyema kuishauri Serikali na Viongozi wenzako ndani ya Chama kuona umuhimu na ulazima wa kuirejesha na kuijenga upya nchi yetu katika misingi ya demokrasia, kuheshimiwa kwa Haki za Binaadamu na uzingatiwaji wa Utawala wa Sheria nchini. " Seif

Ameongeza "Ni wajibu wetu kama Viongozi kuweka mbele na kutanguliza maslahi mapana ya Taifa letu kwa kusimamia Uadilifu, Haki na Uzalendo".

Pamoja na hayo, Chama hicho kimemtakia mapumziko mema Katibu Mkuu mstaafu Ndg, Abdulrahman Kinana kutokana na uamuzi wake wa kustaafu utumishi katika medani ya kisiasa na kwamba wataendelea kukumbuka mchango wake katika ujenzi na ustawi wa Misingi ya Demokrasia hapa nchini.

Source: EATV
Maalim Seif ampatia majukumu Dkt. Bashiru Maalim Seif ampatia majukumu Dkt. Bashiru Reviewed by Zero Degree on 5/31/2018 04:45:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.