Mugabe agoma kwenda kuhojiwa mbele ya kamati ya Bunge
Aliyekuwa rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe |
- Soma na hii - Mugabe atakiwa kufika mbele ya kamati ya Bunge
“Tulimwandikia barua rais huyo wa zamani mara mbili ili aje lakini hakufanya hivyo, sasa tutamwandikia mara ya mwisho kama inavyotakiwa na sheria,” alisema Mbunge Themba Mliswa.
Uchunguzi huo ulioelezewa na gazeti la serikali la Herald kuwa unahusu upotevu wa Dola bilioni 15, (sawa na zaidi ya Tsh. Trilioni 34.2) unatafuta ufafanuzi kutoka kwa Mugabe kuhusu mapato ya almasi yenye thamani hiyo yaliyopotea wakati wa utawala wake.
- Soma na hii - Mugabe hatarini kunyimwa marupurupu yake
Kamati hiyo imesema itatoa wito wa mwisho akitakiwa afike mbele yake Juni 11 mwaka huu. Wito wa kwanza ulimtaka afike mbele yake Mei 23 tatu asubuhi ambapo hakufika kutokana na kile alichosema Mliswa kwamba ilionekana haikuwa vyema kwa mtu wa umri wake kumtaka afike mbele ya kamati hiyo mapema asubuhi.
Alipoulizwa ni hatua gani zingechukuliwa iwapo Mugabe atakataa tena wito huo, Mliswa alisema akipuuza wito huo mara ya tatu, watatafuta msaada wa polisi. Wito wa pili ulikuwa afike kwenye kamati hiyo Mei 28 mwaka huu saa nane mchana lakini kiongozi huyo aliyeitawala nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, hakufika.
- Soma na hii - Aliyemtunuku Grace Mugabe shahada ya uzamifu akamatwa
Mbali na kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani Novemba mwaka jana, kamati hiyo imewaita mawaziri wa zamani, wa sasa na maofisa wa usalama waliohusika na uchimbaji wa almasi ili kupata ufafanuzi zaidi.
Mugabe agoma kwenda kuhojiwa mbele ya kamati ya Bunge
Reviewed by Zero Degree
on
5/29/2018 07:35:00 AM
Rating: