Loading...

Nyota Arsenal ashauriwa kujiunga na Crystal Palace kama ataondoka Emirates


Kiungo wa klabu ya Arsenal, Jack Wilshere amekuwa akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto, huku akiwa hajasaini mkataba mpya Emirates. Mkataba wake wa sasa uko karibuni kuisha na atabaki kuwa mchezaji huru.
Wilshere, ambaye amekuwa katika klau hiyo tangu akiwa na umri wa miaka 9, ameweka wazi kwamba anapendelea kusalia katika klabu yake ya utotoni. Arsenal imempa ofa ya mshara wa pauni 90,000 kwa wiki, ambao ni pungufu ya mshahara wake wa sasa wenye thamani ya karibu pauni 110,000 kwa wiki lakini bado hajalikubali dili hilo.
Licha ya kudaiwa kuwa alikuwa akifanya mazungumzo juu ya mkataba wake kwa kipindi flani, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26 anaendelea kuhusishwa na vilabu kadhaa ambavyo vina nia ya kumsajili akiwa kama mchezaji huru.
Aliyekuwa nyota wa klabu ya Crystal Palace, Clinton Morrison amemshauri kiungo huyo ajiunge na klabu hiyo na anaamini ni klabu sahihi kwake. Ana matumaini pia klabu yake ya zamani itaonyesha nia ya kumsajili Muingereza huyo.

Jack Wilshere
Taarifa ya Express Sport inadai mkongwe huyo wa Crystal Palace alipoulizwa kama angeweza kumsajili endapo angepeata nafasi, alisema: “Kwa asilimia mia moja, ningemsajili Jack Wilshere hata kesho.

“Nafikiri na yeye ni miononi mwa mchezaji mwenye uwezo. Kama ungweza kuwa naye bila majeruhi mara kwa mara, utakuwa ni usajili wa aina yake kwa Crystal Palace.

“Ni wazi kuwa ni mkazi wa London, hivyo pengine anataka kusalia London na knafikiri Crystal Palace itakuwa klabu sahihi kwake.
“Na pengine kama Steve Parish anaweza kufanya dili hilo litokee, ingekuwa jambo zuri sana kama Roy Hodgson angekuwa na nia ya kumsajili.

“Lakini sijui kwanini usimhitaji Jack Wilshere. Wakati anapokuwa bila majeruhi ya mara kwa mara, nafikiri bado ana uwezo mkubwa na ni kiungo mzuri sana.”
    Nyota Arsenal ashauriwa kujiunga na Crystal Palace kama ataondoka Emirates Nyota Arsenal ashauriwa kujiunga na Crystal Palace kama ataondoka Emirates Reviewed by Zero Degree on 5/14/2018 07:35:00 AM Rating: 5

    Powered by Blogger.