Loading...

Nyota Chelsea kuzigonganisha Barcelona, Real Madrid na Juventus


Chipukizi wa klabu ya Chelsea, Callum Hudson-Odoi anazivutia klabu nyingi barani Ulaya, ikiwemo Barcelona, Real Madrid pamoja na Juventus.

Nyoya huyo mwenye umri wa miaka 17 amecheza michezo minne chini ya Antonio Conte msimu huu, miwili ikiwa ni ya Ligi Kuu ya Uingereza.

Hudson-Odoi pia alishinda Kombe la Dunia U17 akiwa na Uingereza mwaka jana, upande aliowakilisha mara 22 kati ya mwaka 2016 na 2017.

Licha ya uwepo wa klabu nyingi zinazomhitaji, Chelsea wanatarajiwa kukataa ofa yoyote itakayotolewa, lakini inatarajiwa kuwepo kwa vita ngumu kama watashindwa kumaliza Ligi Kuu katika nne bora.

Mafanikio ya Jadon Sancho hivi karibuni akiwa Borussia Dortmund kwenye Bundesliga yanawavutia vijana wengi wa Ligi Kuu ya Uingereza kujaribu kutoka nje kutafuta kutambulika.

Callum Hudson-Odoi 
Hata hivyo, Hudson-Odoi amekuwa na mafanikio makubwa akiwa na timu ya vijana ya Chelsea, huku klabu ikifanikiwa kushinda katika hatua ya U18, na anaweza kushawishika kubaki.
Nyota Chelsea kuzigonganisha Barcelona, Real Madrid na Juventus Nyota Chelsea kuzigonganisha Barcelona, Real Madrid na Juventus Reviewed by Zero Degree on 5/08/2018 06:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.