Loading...

Nyota Ligue 1 anaweza kuitosa Liverpool na kujiunga na wapinzani wao


Nyota wa Ligue 1, Nabil Fekir anawindwa sana na vilabu vikubwa vya Ligi Kuu ya Uingereza.

Liverpool, Chelsea na Arsenal wamekuwa wakihusishwa na mshambuliaji huyo wa klabu ya Lyon katika miezi ya hivi karibuni.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na wakati mzuri kwenye Ligue 1 msimu huu na kwa mujibu wa ripoti mbali mbali, kiungo huyo alikuwa anatarajiwa kutua Anfield baada ya kusemwa kuwa amefikia makubaliano nao.

Fekir amekanusha taarifa hizo kwamba anakaribia kusaini mkataba na Liverpool, kitu ambacho kitafungiua milango kwa Chelsea au Arsenal kujaribu bahati yao kwenye majira ya joto.

Nabil Fekir
Fekir alisema: “Sijakaribia kwenda Liverpool. Kuna mazungumzo na vilabu kadhaa yanaendelea lakini nitachukuwa muda wangu kufikiria hilo.

Hili linaweza kuwa pigo kubwa kwa vigogo hao walioshindwa kutamba mbele ya Real Madrid kwenye fainali ya Ligi ya Mabinwga kwenye mbio za kuwania saini ya nyota huyo kutoka Ufaransa.
Nyota Ligue 1 anaweza kuitosa Liverpool na kujiunga na wapinzani wao Nyota Ligue 1 anaweza kuitosa Liverpool na kujiunga na wapinzani wao Reviewed by Zero Degree on 5/29/2018 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.