Loading...

Putin aapishwa kuwa rais wa Urusi kwa muhula wa nne


Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa kwa muhula wa nne kama rais wa Urusi leo Jumatatu baada ya kushinda uchaguzi mnamo Machi.

Amekuwa madarakani kwa miaka 18 kama rais na hata waziri mkuu, na wapinzani wameufananisha muda wake wa uongozi kama utawala wa mfalme.

Polisi wa kupambana na fujo walikabiliana na waandamanaji wanaopinga utawala wake mjini Moscow na katika miji mingine Jumamosi.

Kumekuwa na hofu kwamba huenda kutazuka ghasia tena leo Jumatau wakati anapoapishwa.

Sherehe hiyo ya kuapishwa kwake itafanyika Kremlin mjini Moscow na huedna ikawa na ya watu wa karibu tu ikilinganishwa na ile ya mwaka 2012, shirika la habari la AFP Linaripoti.

Putin anatarajiwa kukutana na watu waliojitolea kushughulika wakati wa kampeni yake peke, shirika hilo la habari linasema.

Rais wa kwanza aliyechaguliwa mnamo mwaka 2000, Putin aliwania tena muhula mwingine mnamo mwaka 2004 kabla ya kujiuzulu 2008 ili kuhudumu kama waziri mkuu chini ya mshirika wake Dmitry Medvedev, kwa sababu kisheria, anaruhusiwa kuhudumu kwa mihula miwili pekee mtawalia.

Ilikuwa wazi ni nani aliye na udhibiti na mwaka 2012 Putin alirudi kama rais, kwa mara hii kwa muhula wa miaka sita.

Iwapo na atakapofika mwisho wa muhula wake wa nne mwaka 2024, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 65 atakuwa amehudumu kwa takriban robo karne madarakani.

Jasusi aliyegeuka kuwa rais

Putin akiwa katika makao makuu ya ujasusi wa kijeshi GRU Moscow mnamo 2006
1952: Alizaliwa Octoba 7 huko Leningrad mji wa pili kwa ukubwa Urusi, akasomea Sheria na kujiunga na Polisi ya KGB akiwa jasusi katika Ujerumani mashariki iliyokuwa na Ukomyunisti

1997: Baada ya kuhudumu kama msaidizi mkuu wa meya wa St Petersburg, akaingia ikulu chini ya Boris Yeltsin akateuliwa kuwa mkuu wa kitengo cha polisi FSB

1999: Alichaguliwa kuwa waziri mkuu , na kuwa kaimu rais baada ya Yeltsin kujiuzulu.

2000: Alichaguliwa Rais na kuhudumu mihula miwili ya miaka minne.

2008: Alizuiwa kuhudumu kwa muhula wa tatu mtawalia, akawashangaza wachambuzi kwa kurudi katika wadhifa wa waziri mkuu huku mshirika wake Dmitry Medvedev akiwa rais

2012: Achaguliwa tena rais na kwa muhula wa miaka sita, chini ya sheria mpya

2018: Achaguliwa kwa muhula wa nne

Urusi imebadilika vipi chini ya utawala wa Putin?

Warusi wa kawaida wamekaribisha utulivu unaotajwa kutokana na miaka ya kwanza ya uongozi wa Puti wakati mfumko wa bei ulidhibitiwa na idara msingi za serikali zilipofufuliwa.

Ghasia za kutaka kujitenga zilizogubika utawala wa kiongozi aliyemtangulia Putin, Boris Yeltsin, hatimaye zilisitishwa kwa umwagikaji damu mkubwa.

Umahiri wake uliozidi ,uliochochewa na ushuru kutoka kwa mafuta gafi na gesi , Bw Putin aliongeza umairi wake uongozini na kusababisha vituo vya habari kurudia nyakati za kale pia uhuru wa kisiasa.

Uamuzi wake wa kuihamisha rasi ya annex Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014 ulizua mgogoro mkubwa tangu vita baridi , na kusababisha vikwazo vinavyoendelea kutoka Magharibi hadi sasa.

Urusi inadaiwa kuingililia kati uchanguzi wa urais wa Marekani 2016 uliozua utata katika mahusiano ya kimataifa.

Mwaka huu Bw Putin aliitupiwa kidole cha lawama na Uingereza kwa shambulio la kemikali kwa jasusi wake - madai ambayo aliyapinga Moscow.

Source: BBC 
Putin aapishwa kuwa rais wa Urusi kwa muhula wa nne Putin aapishwa kuwa rais wa Urusi kwa muhula wa nne Reviewed by Zero Degree on 5/07/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.