Loading...

Serikali yaichambua kazi ya Msajili wa vyama vya siasa


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde amesema kuwa msajili wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria inampa mamlaka ya kuvilea vyama vya siasa pale panapo tokea matatizo.

Akizungumza leo Mei 7 Bungeni jijini Dodoma kwa Niaba ya Waziri Mkuu, Mavunde ambapo amesema kuwa panapo tokea matatizo awe sehemu ya kusaidia vyama hivyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge kuhoji, ni kwanini Msajili anaingilia mwenendo wa vyama vya siasa hali yakuwa vinafanya kazi zake Kikatiba kwa kufanya maamuzi kupitia ofisi ya Msajili na kukataa maamuzi ya vyama vya siasa kama vile chama cha wananchi CUF.

“Msajili wa vyama vya siasa kwa mujibu wa sheria, ukisoma sheria ya vyama vya siasa sura namba 258 iliyolejewa mwaka 2002 na sheria ya vyama vya siasa iliyofanyiwa mabadiliko namba 7 mwaka 2009 inampa mamlaka msajili kuvile vyama vya siasa, panapotokea matatizo awe sehemu ya kusaidia kurudisha harmony akiwa kama mlezi wa vyama vya siasa,” amesema Mavunde.
Serikali yaichambua kazi ya Msajili wa vyama vya siasa Serikali yaichambua kazi ya Msajili wa vyama vya siasa Reviewed by Zero Degree on 5/07/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.