Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 7 Mei, 2018

Nabil Fekir
Lyon wameripotiwa kuwa wamekubali kumuuza Nabil Fekir kwenda Liverpool kwa dili la uhamisho ambalo linakadiriwa kuwa na thamani ya karibu pauni milioni 61.7. (RMC Sport)

Paris Saint-Germain walitaka kumsajili Ryan Sessegnon, lakini beki huyo wa Liverpool anapendelea kwenda Tottenham. (Le10Sport)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameripotiwa kukubali uhamisho wa Anthony Martial kwenda Juventus.

Wakala ameliweka shakani, dili la Jose Mourinho la uhamisho wa kiungo wa klabu ya Lazio, Sergej Milinkovic-Savic kwa pauni milioni 80. (Express)

Golikipa wa Stoke City, Jack Butland ameuelezea na kuufananisha utaratibu wa ajira katika klabu hiyo kama kinyago.

Antonio Conte amesema kuwa Chelsea itaendelea kupambana hadi mwisho wa msimu, licha ya kuwa na wakati mgumu msimu huu.
 
Mshambuliaji wa Celtic, Odsonne Edouard anatarajiwa kuikosa fainali ya Kombe la Shirikisho la Uskoti. (Sky Sports)
 
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amemuonya Mohamed Salah asibweteke na kuanza kujiangusha mchezoni. (Guardian)

Simon Mignolet
Golikipa wa Liverpool, Simon Mignolet anaweza kuondoka Anfield kwenye majira ya joto, huku Borussia Dortmund ikiripotiwa kuwa na hamu ya kumsajili Mbelgiji huyo.

Steven Gerrard anataka kumfanya mshambuliaji wa Liverpool, Dominic Solanke kuwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili akiwa na Rangers. (Sun)

Klabu ya Stoke City inatarajiwa kupoteza wachezaji wengi baada ya kushuka daraja Ligi Kuu ya Uingereza. (Daily Mail)

Inaonyesha Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) litamhoji Mark Hughes aelezee maoni yake aliyotoa kuhusiana na mwamuzi Jon Moss baada ya Southampton kunyimwa ushindi wa muhimu dhidi ya Everton.

Rafa Benitez amemtaka mmiliki wa klabu ya Newcastle, Mike Ashley 'alezee matarajio ya klabu' kabla ya kuanza mipango ya msimu ujao. (Telegraph)

Roy Hodgson ameahidi kuwa Crystal Palace itakuwa msitari wa mbele kumsajili  Ruben Loftus-Cheek kutoka Chelsea kwenye majira ya joto. (Independent)

Leicester watatfuta uweuzekano wa kumteua David Wagner kuwa meneja wao mpya kwenye majira ya joto. (Times)

Liverpool inaongoza mbio za kuwania saini ya golikipa chipukizi wa timu ya taifa ya Ukraine, Andriy Lunin, 19.

Christian Benteke
Crystal Palace wako tayari kusikiliza ofa zitakazowafikia kwa ajili ya uhamisho wa Christian Benteke kwenye majira ya joto. (Mirror)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 7 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 7 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/07/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.