Sarri kutua na straika huyu kama atajiunga na Chelsea
Maurizio Sarri akiwa na klabu ya Napoli |
Kwa mujibu wa taarifa ya Sportsmail, Chelsea wanatarajia kufanya majadiliano na Napoli kuhusu mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 59 kuchukua nafasi ya Antonio Conte Stamford Bridge wiki hii.
Sarri tayari ameshafikia makubaliano binafsi na Chelsea lakini pande hizo mbili bado zinatakiwa kufuata taratibu zilizopangwa na kulipia fedha ya kuvunja mkataba wake, akiwa ameondoka Napoli wiki jana kutafuta nafasi ya kutua London.
Gonzalo Higuain |
- Soma na hii - Sababu ya Conte kutaka kuondoka Chelsea yabainika
Inadaiwa mashambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina ana ukaribu mkubwa sana na Sarri na alifurahia msimu bora zaidi chini ya uongozi wake katika klabu ya Napoli.
Higuain aliandika rekodi mpya Serie A kwenye msimu wa 2015/16 ya kufunga magoli 36 ndani ya michezo 35 kabla hajaondoka kwenda Juventus kwa pauni milioni 75.
Wawili hao wameonyesha tamaa ya kufanya kazi pamoja tena na wazo hilo la wao kukutania katika klabu ya Chelsea linaanza kusikika.
Sarri tayari ameshaanza kufanya mipango ya usajili na amemtaja Higuain kama chaguo lake la kwanza.
Uhamisho wa Higuain kwenda Stamford Bridge unaweza kutoa njia pia kwa Alvaro Morata kuondoka katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda katika klabu yake ya zamani, Juventus baada ya kuwa na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Uingereza uliomsababishia aachwe nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia.
Sarri pia atatazamia kuja na beki Kalidou Koulibaly kutoka Napoli, lakini Chelsea inaweza kushindwa kumnasa Msenegali huyo kutokana na thamani yake kubwa ya pauni milioni 80.
Uhamisho wa Higuain kwenda Stamford Bridge unaweza kutoa njia pia kwa Alvaro Morata kuondoka katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Chelsea amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda katika klabu yake ya zamani, Juventus baada ya kuwa na msimu mbaya katika Ligi Kuu ya Uingereza uliomsababishia aachwe nje ya kikosi cha timu ya taifa ya Uhispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia.
Kalidou Koulibaly |
Sarri kutua na straika huyu kama atajiunga na Chelsea
Reviewed by Zero Degree
on
5/28/2018 07:05:00 AM
Rating: