Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 30 Mei, 2018

Mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale
Tottenham wako tayari kutoa ofa kubwa ambayo inaweza kuiweka Manchester United kando kwenye mbio za kuwania saini ya, Gareth Bale kutoka klabu ya Real Madrid.

Kwa mujibu wa taarifa ya AS Roma, Liverpool hawajapeleka ofa ya kwa ajili ya golikipa wao, Alisson Becker.

Kiungo mpya wa Liverpool, Fabinho anasema kuwa Klopp na Firmino ndio waliomshawishi kwenda Anfield. (ESPN)

Manchester United wanatarajiwa kukamilisha usajili wao wa kwanza kwenye majira haya ya joto kwa kumnasa beki wa kulia wa Porto, Diogo Dalot.
 
Klabu ya Everton itamteua rasmi Marco Silva kuwa meneja wao mpya wiki hii achukue nafasi ya Sam Allardayce.

Paul Hurst ameondoka Shrewbury kwenda kuwa meneja mpya wa klabu ya Ipswich Town. (talkSport)

Roma watataka walipwe pauni milioni 80 ili kumwachia golikipa anayewindwa na Liverpool pamoja na Real Madrid, Alisson Becker. (Guardian)

Manchester City watakamilisha usajili wa mshambuliaji wa Leicester, Riyad Mahrez kwa pauni milioni 75 wiki hii. 

Maurizio Sarri
Dili la Chelsea kumteua Maurizio Sarri linakaribia kugonga mwamba kufuatia klabu ya Napoli msistizo wa kulipwa pauni milioni 7 ili kuvunja mkataba wa kocha huyo. (Express)

Ramsey hana mapango wa kuondoka Arsenal na ana shauku kubwa ya kuanza msimu mpya chini ya uongozi mpya wa Unai Emery, huku akisifia kuwasili kwa Mhispania huyo katika dimba la Emirates.

Baba mzazi wa Christia Pulisc amewaomba mashabiki kuzipuuza tetesi ambazo zinamhusishwa mwanae na klabu za Tottenham, Liverpool na Man United. 

Nahodha wa timu ya taifa ya Brazil, Thiago Silva amesema kuwa Mbrazil mwenzake, Fabinho atakuwa na mafanikio makubwa Uingereza.

Kwa mujibu wa wakala wa Robert Lewandowski, mshambuliaji huyo wa Bayern Munich aliambia klabu yake kuwa ana lengo la kundoka akatafute changamoto mpya. (Sky Sports)  

Manchester United na Chelsea watashindania kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba, kwa mujibu wa ripoti za nchini Uhispania.

Rafa Benitez anaweza kupata pauni milioni 30 za ziada kutumia, klabu yake ikiwa imemruhusu Aleksandar Mitrovic kwenda Fulham, kuwauza Chancel Mbemba na Mats Sels kwenda Anderlecht na kumpa Mikel Merino nafasi ya kurejea uhispania.

Mtikisoko katika benchi la ufundi la Unai Emery unaweza kuwa na maana kuwa mwisho wa wakongwe wa Arsenal, Steve Bould na Jens Lehmann umefika.

Riyad Mahrez 
Manchester City wanatarajiwa kumsajili Riyad Mahrez kwa bei ya kati - lakini bado itavunja rekodi yap ya usajili.

Ashley Young anasema kuwa mgogogro wake na mchezaji mwenzaje wa Uingereza, Dele Alli umeshaisha muda mrefu. (Sun)

Arsenal bado wa matumaini ya kuwasajili Sokratis Papastathopoulos, Stephan Lichtsteiner na Caglar Soyuncu kabla Kombe la Dunia halijaanza.

Tottenham wanafikiria kumsajili golikipa wa Southampton, Alex McCarthy kama mtu sahihi wa kuweza kumsaidia golikipa wao namba moja, Hugo Lloris.

Lazio wanategemea kumpoteza Sergej Milinkovic-Savic kwenda klabu kubwa inayoshiriki Ligi ya Mabingwa kwenye majira ya joto lakini hawana mpango wa kumuuza kwa bei ndogo. (Mirror)

Beki wa Hull City, Michael Dawson anakaribia kurejea katika klabu yake ya utotoni, Nottingham Forest. (Daily Mail)

Fulham wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 9 kwa ajili ya beki wa klabu ya Bristol City, Aden Flint pamoja na kuwasajili kwa mkopo Matt Targett kutoka Southampton na Aleksandar Mitrovic wa Newcastle. (Star)

Viongozi wa FA wamethibitisha hadharani kwa mara ya kwanza kwamba Ligi Kuu ya Uingereza itakuwa na kindi kifupi cha mapumziko kwenye majira ya baridi. (Times)

Phil Foden
Man City hawatamtoa Phil Foden kwa mkopo msimu ujao, huku wakijiandaa kutangaza dili mkataba mpya kwa chipukizi huyo. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 30 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 30 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/30/2018 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.