Loading...

Kocha Simba alia na ratiba ya Ligi Kuu


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amelalamika juu ya ratiba ambayo wanaipitia kwa sasa ya kucheza mechi tatu ndani ya siku nane kwa kuwa haitoi muda wa kupumzika kwa wachezaji wake.

Aussems amesema kuwa ratiba kwao haijakaa sawa kwani inaweza kusababisha majeraha kwa wachezaji wake kwa kushindwa kutoa muda wa mapumziko baada ya kumaliza mechi moja.

"Kwa sasa tuna ratiba ngumu kidogo, kwani ndani ya muda mfupi tunacheza mechi tena, utaona tumecheza jumapili iliyopita, baada ya siku chache tunacheza tena na baada ya hapo tunacheza tena,kitu hicho ni kigumu kinaweza kusababisha matatizo kwa wachezaji," alisema.

Simba kuanzia Jumapili iliyopita hadi jumapili hii watakuwa na mechi tatu tofauti, walianza kupambana na Stand United wiki iliyopita, leo watacheza na Alliance na jumapili watacheza na Ruvu Shooting.
Kocha Simba alia na ratiba ya Ligi Kuu Kocha Simba alia na ratiba ya Ligi Kuu Reviewed by Zero Degree on 10/24/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.