Loading...

Ronaldo amtembelea Sir Alex Ferguson baada ya Juve kuiua Man U


Nyota wa klabu ya Juventus na taifa la Ureno Cristiano Ronaldo amemtembelea aliyekuwa kocha wake wa zamani na klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson na kummwagia sifa kedekede.

Ronaldo amekutana na Ferguson leo baada ya kumaliza mchezo wao dhidi ya klabu ya Manchester Unoted katika dimba la Old Trafford katika michuano mikubwa kabisa ya UEFA Champions League ambao ulimalizika kwa Juventus kuondoka na ushindi mwembemba wa goli moja.


Kabla ya kukutana na Ferguson Ronaldo aliongea juzi kabla ya mchezo ambapo ilikuwa ni safari yake ya pili kurudi katika uwanja huo tangu aondoke Manchester kwani mara ya kwanza alirudi ambapo alikuwa Real Madrid na kipindinkile alifanikiwa kufunga goli lakini awamu hii hakufanikiwa kupata goli licha ya kucheza na kutengeneza nafasi nyingi za magoli.

Katika mkutano huo alioongea na waandishi wa habari Ronaldo aliongea na kuusifia uwanja huo na kusema “Kurudi kwangu hapa inanikumbusha vitu vingi sana ikiwemo mataji furaha,upendo kutoka kwa aliyekuwa kocha wangu Ferguson ambaye ni kocha bora kwangu ni kocha bora wa muda wote”


Safari hii yaonaldo kukutana na Fergson ni kwa mara ya kwanza tangu mzee huyo kufanyiwa operesheni ya kichwa miezi kadhaa nyuma na kipindi hicho Ronaldo aliongea nkuoyeshwa kuumizwa na kitendic cha Ferguson kufanyiwa upasuaji huo.

Kwa mara hii Ronaldo ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa “Kocha bora zaidi na juu ya yote ni mtu mzuri. Alinifundisha mimi mambo mengi sana ndani na hata nje ya uwanja, nimefurahi kukuona ukiwa katika hali nzuri”


Ronaldo amtembelea Sir Alex Ferguson baada ya Juve kuiua Man U Ronaldo amtembelea Sir Alex Ferguson baada ya Juve kuiua Man U Reviewed by Zero Degree on 10/24/2018 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.