Loading...

Makonda atangaza fursa kwa wataalamu wa IT


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, anawaalika wote wenye utaalam wa Teknolojia ya Habari yaani (Information Technology – IT specialists) kufika ofisini kwake Novemba 1, 2018, asubuhi kwa ajili ya kuunda Mfumo wa Kuratibu Uwajibikaji wa Watendaji wa Umma ili kuhakikisha malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa uharaka.

Mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya mitaa, kata, wilaya, mikoa na viongozi wakuu akiwemo mkuu wa mkoa, katibu tawala mkoa, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara, ambapo watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiyewajibika kutatua kero za wananchi.

Makonda amesema hataki kuona wananchi wanafika kwenye ofisi za umma na kuambiwa “Njoo kesho” kila siku pasipokujua kuwa wanatumia nauli na kupoteza muda.

Mfumo huo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.

SHAUKU YA RC MAKONDA NI KUONA UWAJIBIKAJI NA UTENDAJI KWENYE OFISI ZA UMMA UNAONGEZEKA ILI KUPUNGUZA KERO KWA WANANCHI.
Makonda atangaza fursa kwa wataalamu wa IT Makonda atangaza fursa kwa wataalamu wa IT Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 05:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.