Loading...

Okwi, Kichuya ruksa kwenda Ubelgiji - Simba SC


Ofisa habari wa timu ya Simba Haji Manara amesema kuwa hawana tatizo na timu ambayo itakuwa inahitaji kumchukua mchezaji yoyote ndani ya kikosi endapo watafuata utaratibu.

Manara ameyasema hayo baada ya nyota wa timu ya Simba Emanuel Okwi na Shiza Kichuya kuhusishwa na kujiunga na moja ya timu inayoshiriki ligi kuu nchini Ubelgiji ambako Mbwana Samatta anachezea timu ya KRC Genk.

"Hakuna klabu ambayo inaweza kumzuia mchezaji kuitumikia timu ambayo anahitajika,hivyo kwetu sisi mchezaji yoyote tunampa ruhusa kujiunga na timu yoyote ambayo itafuata utaratibu wa kumsajili"alisema.
Okwi, Kichuya ruksa kwenda Ubelgiji - Simba SC Okwi, Kichuya ruksa kwenda Ubelgiji - Simba SC Reviewed by Zero Degree on 10/22/2018 05:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.