Mwili wa Isaac Gamba wawasili Dar
Mwili wa Gamba ukiwasili Airport |
- Soma na hii - Historia ya marehemu Isaac Nyagabona Muyenjwa Gamba
Watu mbalimbali wamejitokeza Uwanjani hapo kuupokea mwili wa Gamba wakiwemo wanahabari ambao alifanya nao kazi kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni hapa nchini, Sam Mahela, Zomboko, Adballah Mwaipaya na wengine.
Baada ya kupokelewa, mwili huo umepelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo ambako ibada na shughuli nzima ya kumuaga marehemu zitaanza leo Jumatatu majira ya saa tano asubuhi na baadaye utapelekwa airport tayari kwa safari kuelekea kwao Bunda kupitia Mwanza kwa ajili ya maziko.
Aidha, wadau wa Mwanza kuanzia saa tano asubuhi kesho katika Viwanja vya Ofisi ya UTPC watapata nafasi ya kumuaga mpendwa Gamba na baadaye msafara wa magari utaondoka kuelekea Bunda kwa mazishi.
Aidha, wadau wa Mwanza kuanzia saa tano asubuhi kesho katika Viwanja vya Ofisi ya UTPC watapata nafasi ya kumuaga mpendwa Gamba na baadaye msafara wa magari utaondoka kuelekea Bunda kwa mazishi.
Gamba alifariki wiki iliyopita jijini Bonn nchini Ujerumani alikokuwa akifanya kazi Zake.
Mwili wa Isaac Gamba wawasili Dar
Reviewed by Zero Degree
on
10/29/2018 08:50:00 AM
Rating: