Loading...

Ngoma atamba kuipa Ubingwa Azam FC


STRAIKA ambaye anarudi kwenye makali yake, Donald Ngoma wa Azam FC ameweka wazi kuwa lengo lake ndani ya kikosi hicho ni kuipambania na kuipatia timu hiyo ubingwa wa ligi kuu kwa msimu huu.

Ngoma ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi 10 kutokana na majeraha kwa sasa anaanza kurudisha makali yake ambapo hivi karibuni alifunga bao lake la kwanza akiwa na jezi za timu hiyo ya Azam kwenye mechi dhidi ya Coastal Union.

Mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa Zimbabwe amesema kuwa kitu ambacho yeye na wachezaji wenzake wanachoangalia hivi sasa ni kupata ushindi kwenye mechi zijazo hadi kuchukua ubingwa wa ligi.

“Tukiendelea kucheza vizuri na kupata pointi nyingine kwenye mechi zetu hilo litafanikisha kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo yetu ya kutwaa ubingwa ambayo tumejiwekea hapa.

“Tunaamini kwamba tutalifanikisha hilo kwa sababu tunataka tuchukue ubingwa, hilo ndiyo jambo tunaloliangalia kwanza,” alisema Mzimbabwe huyo.
Ngoma atamba kuipa Ubingwa Azam FC Ngoma atamba kuipa Ubingwa Azam FC Reviewed by Zero Degree on 10/17/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.