Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Octoba, 2017

Raheem Sterling
Real Madrid wanatarajia kuimarisha mkakati wao wa kusaka saini ya Raheem Sterling kufuatia uwezo ambao nyota huo ameonyesha tangu kuanza kuwa msimu huu.

Paul Scholes anadai Manchester United imeshuka kiwango sana kiasi kwamba hata Lionel Messi mwenyewe angepata wakati mgumu kucheza Old Trafford chini ya Jose Mourinho.

Celtic wamekanusha ripoti zinazodai kwamba Daniel Arzani anarejea Manchester City kabla mkataba wake wa mkopo haujaisha.

Wawekezaji wa Kimarekani wako tayari kutoa ofa ya hadi pauni milioni 300 kwa ajili ya kuinunua klabu ya Newcastle lakini dili hilo liko hatari kufa, huku kukiwa na hofu ya klabu hiyo kushuka daraja. (Daily Mail)

West ham ina mpango wa kurejea sokoni mwezi Januari kuisaka saini ya nyota wa Argentina, Franco Vazquez baada ya jaribio lao kugonga mwamba kwenye majira ya joto. (talkSport)

Jamie Carragher anasema kwamba macho yote yatamtazama Jose Mourinho kwenye mchezo wa Manchester United na Chelsea Jumamosi.

Klabu ya Swansea imethibitisha kwamba Wilfred Bonny amerejea mazoezini akitokea kuuguza majeraha yake aliyopata mwezi Februari.

Brentford wamemteua Thomas Frank kuwa meneja wao mpya. (Sky SPorts)

Klabu ya Barcelona inatazamia kumpa ofa ya mkataba mfupi aliyekuwa beki wa klabu ya Chelsea, Branslav Ivanovic, 34 anayeichezea klabu ya Zenit Saint Petersburg.

Neymar Jr
Nyota wa klabu ya PSG na timu ya taifa ya Brazil, Neymar yuko tayari kurejea katika klabu yake ya zamani, Barcelona na hali inaonyesha klabu hiyo ya La Liga iko tayari kumfikiria. (El Mundo Deportivo)

Manchester United sasa italipa kipaumbele suala la mkataba mpya wa David de Gea baada ya kupiga hatua kubwa katika mazungumzo ya mikataba mipya ya Luke Shaw na Anthony Martial.

Marcos Alonso amesema kuwa anajiandaa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Chelsea "siku chache zijazo". (Evening Standard)

Jose Mourinho ameitaka klabu ya Manchester United kushughulikia suala la mikataba mipya ya Juan Mata na Ander Herrera. (Star)

Everton imejiunga na mbio za kuwania saini ya Aaron Ramsey na wanaweza kutoa ofa ya mshahara wa pauni 150000 kwa wiki kwa kiungo huyo wa Arsenal.

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kuanza mchakato wa kuisaka saini ya nyota wa klabu ya Ajax, Frenkie De Jong anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 80.

Bournemouth ina mpango wa kufanya mazungumzo ya mkataba mpya na winga wa klabu hiyo, Ryan Fraser.

Manchester City wamepata pigo baada ya Danilo kuondoka uwanjani akiwa majeruhi wakati Brazil ilipocheza dhidi ya Argentina.

PSG wanafuatilia kwa karibu zaidi mazungumzo ya mkataba mpya  wa Raheem Sterling.

Burnley wanaweza kumpa Mark Warburton nafasi ya kurejea kwenye tasnia ya soka - kama mkurugenzi wao wa kandand. (Sun)

Michael Essien na Jose Mourinho
Michael Essien anasema kuwa bado ni shabiki namba moja wa Jose Mourinho na anaamini mreno huyu anaweza kufanya mabadiliko Manchester United.

Barcelona imemkingia kifua Lionel Messi kwenye vita yake ya maneno na raia mwenzake wa Argentina, Diego Maradona. (Mirror)

Kiwango alichoonyesha Raheem Sterling akiwa na timu ya taifa ya Uingereza kimeichochea klabu yake ya Manchester City kuhitaji kufanya mazungumzo naye ya mkataba mpya, huku akiendelea kuhusishwa na Real Madrid.

Jose Mourinho anatarajiwa kuwa kwenye benchi la ufundi wakati Manchester United itakapoifuata Chelsea licha ya kushitakiwa na FA.

Mwenyekiti wa klabu ya Chelsea, Bruce Buck ameibuka na kudai kwamba atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha Eden Hazard anaongeza mkataba Stamford Bridge.

Wakala wa Krzysztof PiÄ…tek amethibitisha kuwa bado hawajapokea ofa rasmi kwa ajili ya mshambuliaji huyo raia wa Poland, huku kukiwa na taarifa ambazo zinamhusisha na uhamisho kwenda klabu ya Chelsea. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 17 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/17/2018 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.