Loading...

Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Prof. Humphrey Moshi kuwa mwenyekiti wa Tume ya Ushindani nchini (The Fair Competition Commission- FCC).

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Oktoba 30 kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema kuwa uteuzi wa Prof. Moshi utaanza rasmi leo Oktoba 30.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Humphrey P.B. Moshi kuwa mwenyekiti wa Bodi ya ushindani", ameandika Msigwa.

Prof. Moshi anachukua nafasi ya Prof. Samwel Wangwe ambaye muda wake umekwisha baada ya kutumikia kwa miaka minne tangu mwaka 2014 alipoteuliwa chini ya serikali ya awamu ya nne na Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Kabla ya uteuzi huo Prof. Moshi alikuwa mhadhiri mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine Reviewed by Zero Degree on 10/30/2018 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.