RC Makonda aonyesha sura ya mtoto wake kwa mara ya kwanza
RC Makonda akizungumzia changamoto alizopitia kwa miaka 7 ndani ya ndoa, amesema ni miujiza tu ya Mungu iliyofanikisha kupata mtoto.
Siku ya leo ni siku kubwa kwangu sababu nimetimiza miaka saba ya ndoa yangu, nikitizama njia tuliyopita bado nawaza tumewezaje kufika tulipo, na ndipo ninapomrudishia MUNGU sifa na utukufu.
"Ni miaka saba ambayo MUNGU ametupa Baraka na zawadi ya kipekee, pamoja na uhai MUNGU aliotupatia lakini kwa wanandoa MTOTO ni moja ya zawadi kubwa ambayo wanandoa huitegemea, huiomba na kumlilia MUNGU usiku na mchana waweze kuipata, leo namshukuru MUNGU ninayo furaha kubwa kusherehekea miaka saba ya ndoa yangu nikiwa na mtoto wa kiume anaejulikana kwa jina la KEAGAN, Namshukuru MUNGU kwasababu haikuwa rahisi, na najua kuna wengine ambao wamekata tamaa ndani ya mwaka mmoja, miaka miwili au mitatu, na wengine hata ndoa zao kuvunjika kwasababu ya kutokupata mtoto, lakini jawabu la MUNGU hutoka kwa wakati wake..
Naendelea kumshukuru sana MUNGU kwa kunipa mke mwema aliepita nami katika mabonde na milima, hata pale Dunia iliponiacha peke yangu, MARIA WANGU hakuthubutu hata kwa sura kuonesha hayuko pamoja na mimi, naendelea kumshukuru zaidi hata niliporudi kazini nikiwa naweweseka sijui hili wala lile alionesha tabasamu na kuniambia MUNGU YUPO, hata hili tutavuka mume wangu’ alinifuta machozi usiku wa manane pale nilipopaza sauti na kumlilia MUNGU nae akiwa pembeni akisema nitasimama na wewe tutaomba pamoja, pale ninapoamka asubuhi na kukuta magazeti yamechafuka na kuandika kila aina ya habari bado mke wangu alisema BADO NAMUAMINI MUNGU HATA HILI ATAKUVUSHA, pale nilipokaa na kuona mitandao ya kijamii ikinisema kwa kila namna na wengine kwenda mbali zaidi na kutoa kila aina ya matusi, lakini bado mke wangu hakuweza kukata tamaa, aliendelea kuniamini, kuniombea na kunishika mkono, amefanyika kuwa jua pale nilipohitaji muangaza, amefanyika kuwa maji pale nilipohitaji, alifanyika kuwa kila unachokijua kuhakikisha kwamba sikati tamaa, na kwa hilo sina zaidi ya shukurani za kipekee kwake, nafahamu hakika umri wangu wa ndoa sio mrefu kuliko wewe na wengine ambao wako katika ndoa miaka kumi, ishirini au thelathini, lakini kwa yake niliyoyapitia inatosha kusema ASANTE MUNGU KWA KUNIPA MKE MWEMA.
Kipenzi changu Maria, wewe ni Jua langu, mwezi wangu , amani yangu, pepo yangu, kipenzi cha
Kwa upande mwingine wasanii wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz amemtumia ujumbe wa kheri RC Makonda kufuatia tukio hilo.
"Wengi wanazaniaga kufurahia miaka mingi ya ndoa ni kufurahia mazuri mlopitia.. lakini pasipokujua siku hii hutumikaga kwa kujipongeza kwa changamoto mbalimbali kama familia mlizozipitia na kuzikabili na still kuendelea kuwa pamoja, kupendana na kuthaminiana kama Roho na Moyo Mmoja… Kupitia familia yenu nimejifunza Vitu 6 Vikuu:-
1. Kufanya kazi kwa Bidii
2.Kumueka mbele Mwenyez Mungu
3.Upendo
4.Uvumilivu
5.Kusamehe
6.Kutosikiliza Maneno ya watu
Happy 7th Anniversary
The Makondas… Asante kwa kutuletea Keagan @baba_keagan 🙏🏻
RC Makonda aonyesha sura ya mtoto wake kwa mara ya kwanza
Reviewed by Zero Degree
on
10/24/2018 09:20:00 AM
Rating: