Loading...

Ajibu anastahili kucheza Ulaya - Chirwa


Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga raia wa Zambia, Obrey Chirwa amefunguka juu ya uwezo wa kiungo mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kusema kuwa kuwa hastahili kuwa bongo labda Ulaya kutamfaa.

Chirwa aliitumikia Yanga msimu uliopita, aliondoka na kujiunga na timu ya Ismailia ya Misri lakini inaelezwa kuwa mambo yake huko sio mazuri anataka kurudi nchini kuitumikia Yanga licha ya kocha Mwinyi Zahera kumkataa.

"Ajibu ni mchezaji mzuri sana na wala sishangai kuona akifanya vizuri msimu huu,sababu nakijua kipaji chake muda mrefu naona akiisaidia Yanga kwa kipindi kirefu naamini kwa kiwango chake anastahili kwenda Ulaya,"alisema.

Ajibu ameonyesha kiwango kikubwa msimu huu kwenye michezo ya Ligi Kuu Bara kwa kuwa mpaka sasa amehusika kwenye mabao 8 ya timu kwa kutoa pasi za mwisho na kufunga mabao 3 idadi inayokamilisha mabao 11.
Ajibu anastahili kucheza Ulaya - Chirwa Ajibu anastahili kucheza Ulaya - Chirwa Reviewed by Zero Degree on 10/24/2018 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.