Watu wawili wamefariki baada ya malori mawili kugongana mkoani Morogoro
Ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa saba imehusisha malori mawili aina ya Scania yenye namba ya usajiri T 247 CMT/T. 807 CMN mali ya kampuni ya Lake Oil iliyogongana na Scania yenye namba za usajili za kugongana T. 430 BLZ/T. 527 BLY.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Mugabo Wekwe amethibitisha kupokea taarifa ya ajali hiyo, iliyohusisha malori hayo mawili na kusema kuwa miili pamoja na majeruhi wamehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Mikumi.
Kamanda Mugabo amewataja waliofariki kuwa ni dereva na utingo wa gari yenye namba T 430 BLZ ambao majina yao bado hayajafahamika na majeruhi ni dereva wa kampuni ya Lake Oil, Ivan Thadei ambaye hali yake bado ni mbaya.
Kamanda Mugabo amewataja waliofariki kuwa ni dereva na utingo wa gari yenye namba T 430 BLZ ambao majina yao bado hayajafahamika na majeruhi ni dereva wa kampuni ya Lake Oil, Ivan Thadei ambaye hali yake bado ni mbaya.
Watu wawili wamefariki baada ya malori mawili kugongana mkoani Morogoro
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2018 07:20:00 AM
Rating: