Ronaldo, Pogba kutengeneza historia UEFA
Mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa timu hizo kukutana tangu mwaka 2003 utashuhudia historia mbalimbali zikiwekwa.
Paul Pogba
Mchezaji ghali zaidi katika kikosi cha Manchester United Paul Pogba, ambaye alinunuliwa kutoka Juventus kwa dau la rekodi ya dunia €105m mwaka 2016 atakuwa anakutana na timu yake ya zamani pamoja na kukabiliana na nyota mwenzake wa Ufaransa.
Ronaldo dhidi ya Man United
Hii ni mara ya pili kwa Cristiano Ronaldo kurejea Old Traford akiwa kama mpinzani baada ya kufanya hivyo akiwa na Real Madrid na sasa Juventus.
Baada ya jana kufika kwenye uwanja wa Old Traford alisema anajisikia furaha na hisia nyingi nzuri na zaidi akimtakia heri kocha Alex Ferguson ambaye alimsaidia kwa kiasi kikubwa kufikia malengo yake.
Ronaldo aliondoka Old Traford mwaka 2009 na kutua Real Madrid ambako ameondoka mwaka huu na kwenda Juventus. Pogba naye aliondoka Man United mwaka 2012 kwenda Juventus na kurejea 2016.
Man United na Juventus zimekutana mara 12 huku kila timu ikishinda mara 5 na zikitoka sare mara 2.

Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2018 09:35:00 AM
Rating: