CCM walitupora jimbo la Liwale - CUF
Magdalena Sakaya, CUF |
Sakaya amesema kuwa kikao hicho kitatoa majibu endapo wataendelea au watajiondoa kwa yale yanayojitokeza kwenye chaguzi zilizopita ikiwemo mawakala wake kutopewa fomu za kusimamia kura katika baadhi ya vituo.
Kwa mujibu wa taarifa ya EATV, Sakaya amesema kuwa uchaguzi uliopita katika jimbo la Liwale CUF walionewa na kuporwa jimbo hilo ambalo lilikuwa ni ngome yao.
"Nilikuwepo Liwale nmeshuhudia kila kitu, CCM wametuibia kura zetu kwani asilimia 75 ya wapiga kura waliipigia kura CUF lakini mawakala wetu walinyimwa fursa ya kusimamia na kuhesabu kura zetu", amesema Sakaya.
Marudio ya uchaguzi wa jimbo la Liwale yalifanyika, Oktoba 13, baada ya aliyekuwa mbunge wake Zuberi Kachauka (CUF) kujiuzulu na kujivua uanachama na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo aliteuliwa kuwa mgombea kupitia chama hicho na baadae kuibuka mshindi katika uchaguzi huo wa marudio.
CHADEMA kupitia mwenyekiti wake wa chama, Freeman Mbowe kilitangaza kujiondoa rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi.

Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2018 09:50:00 AM
Rating: