Loading...

Rais Magufuli, Kikwete wateta Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akiwa na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es salaam.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu imesema kuwa Kikwete na Rais Magufuli wamekutana kwa utaratibu wa kawaida wa kusalimiana na kutakiana heri katika majukumu.

Akizungumza baada ya kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Kikwete amesema kuwa, "Nimekuja kusalimiana na kumtakia kila la kheri anafanya kazi nzuri, aendelee tu kuchapa kazi na sisi tupo kwa namna yoyote ya kumpa nguvu tupo tayari kumsaidia", amesema Rais mstaafu Kikwete.

Mapema Agosti 15, Rais Dkt. John Magufuli alimteua Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete kumwakilisha katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa zitakazofanyika mjini Harare.
Rais Magufuli, Kikwete wateta Ikulu Rais Magufuli, Kikwete wateta Ikulu Reviewed by Zero Degree on 10/23/2018 12:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.