Yanga yakaribia kunasa beki kutoka Rayon ya Rwanda
Usajili wa beki huyo katika kikosi cha Yanga unaonekana upo karibu kukamilika, wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufunguliwa wiki mbili zijazo, Novemba 15.
Yanga imemtengea beki huyo kitita cha dola 40,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh milioni 91. Taarifa za jana zilisema Simba nao wameingilia usajili huo, lakini kocha wake Patrick Aussems ameliambia gazeti hili kuwa hana haja ya kusajili mchezaji yeyote kwa sasa.
Beki huyo, hivi karibuni alifuatwa na viongozi wa Yanga na kuzungumza naye wakati timu hiyo ilipocheza na Rayon katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, uliochezwa Rwanda.
Yanga imepanga kusajili wachezaji watatu wa kimataifa katika usajili wa dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Novemva 15, mwaka huu ambao ni beki wa kati, kiungo na mshambuliaji.
Vyombo vya habari vya nchini Rwanda, tayari vimeanza kuripoti Yanga na beki huyo mwenye umbo kubwa kufikia muafaka mzuri.
Vyombo hivyo vya habari tayari vimeanza kuthibitisha beki huyo kumalizana na Yanga ambaye kama yeye akitua Jangwani itafikisha idadi ya mabeki wanne wa kati, wakiongozwa na Kelvin Yondani, Vicent Andrew ‘Dante’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
Vyombo hivyo vya habari tayari vimeanza kuthibitisha beki huyo kumalizana na Yanga ambaye kama yeye akitua Jangwani itafikisha idadi ya mabeki wanne wa kati, wakiongozwa na Kelvin Yondani, Vicent Andrew ‘Dante’ na Abdallah Shaibu ‘Ninja’.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika kuzungumzia hilo, alikiri kuwepo mazungumzo ya mwisho ya kukamilisha usajili wa beki huyo wa kati huku akificha dau lake la usajili.
“Tupo kwenye mazungumzo na mabeki wawili wa kati akiwemo Rwatubyaye wa Rayon ambaye yeye ana nafasi kubwa ya kutua kuichezea Yanga kama mazungumzo yakienda vizuri.
“Atatua kuichezea Yanga katika usajili wa dirisha dogo msimu huu, ni kati ya mabeki bora tuliowaona viongozi, hivyo tusubirie kama mambo yakienda vizuri kwa maana ya kukamilisha usajili wake, basi tutaweka wazi kila kitu,” alisema Nyika.
Yanga yakaribia kunasa beki kutoka Rayon ya Rwanda
Reviewed by Zero Degree
on
10/30/2018 10:20:00 AM
Rating: