Leicester City kubadili jina la uwanja
Uwanja wa Leicester City, King Power |
Mmiliki huyo wa Leicester City na wengine wanne wameripotiwa kufariki katika ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo, ajali iliyotokea Jumamosi ya Oktoba 27 baada ya kumalizika kwa mchezo wa EPL kati ya Leicester City na West Ham United, mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 .
Mtoto wa tajiri huyo aitwaye, Aiyawatt ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Leicester City ndiye atakayechukua nafasi yake kwa muda, ambapo anatarajia kukutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa klabu, Susan Whelan kuhusiana na namna nzuri ya kumuenzi mmiliki huyo wa klabu.
"Uwanja wa King Power ni matokeo ya mafanikio kutokana na uwekezaji wa Khun Vichai, tutafungua rasmi majadiliano na familia, klabu na mashabiki kwaajili ya jina la uwanja wetu, litakalomuenzi Khun Vichai", imesema taarifa ya klabu hiyo.

Reviewed by Zero Degree
on
10/30/2018 10:05:00 AM
Rating: