Beki ajitoa Simba SC kisa benchi
Mlipili alijiunga na Simba msimu uliopita akitokea timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza, anadaiwa kutimka zake katika kikosi hicho yapata wiki sasa.
Habari kutoka ndani ya Simba ziliezleza kuwa baada ya kuona hana nafasi ndani ya kikosi cha timu msimu huu tofauti na msimu uliopita ambao alikuwa yupo kikosi cha kwanza.
"Hata viongozi hawajui alipo kwa sababu kaondoka bila kutoa taarifa na sasa yapata wiki, mazoezi yote tuliyofanya ya kujiandaa dhidi ya Alliance FC, Stand United pamoja na Ruvu Shooting hakuwepo," kilieleza.
Kocha Mkuu Patrick Aussems alisema kuwa hana taarifa zake hivyo hawezi kumzunguzia mchezaji huyo.
Beki ajitoa Simba SC kisa benchi
Reviewed by Zero Degree
on
10/30/2018 09:50:00 AM
Rating: