Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Januari 31, 2019
Kocha Chelsea Maurizio Sarri amesema kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, anaweza kuondoka Chelsea kama atataka mwishoni mwa msimu.
Klabu ya West Ham pia inamtaka Batshuayi ambaye ni raia wa Ubelgiji, lakini ni kwa mkataba wa mkopo.
West Ham wamekataa kitita cha pauni milioni 7 kutoka Valencia kwa usajili wa mshambuliaji wa Mexico Javier Hernandez, 30. (Sky Sports)
Paris St-Germain wametoa ofay a dakika za mwisho ya kutaka kumsajili kwa mkopo mchezaji wa Arsenal, Mjerumani Mesut Ozil, 30. (Metro)
PSG pia wanataka kumsajili winga wa Chelsea na Brazil Willian, 30, kwa mkopo kama mbadala wa Neymar ambaye ni majeruhi.
West Ham wamefanya mazungumzo na Chelsea wakitaka kujua uwezekano wa kumsajili streka wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 32. (Mail)
West Ham wamefanya mazungumzo na Chelsea wakitaka kujua uwezekano wa kumsajili streka wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 32. (Mail)
West Ham pia wanamuwinda kiungo wa Chelsea Danny Drinkwater, 28, ili wamsajili kwa mkopo. (Talksport)
Everton wanataka kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, ambaye amechezea raundi ya kwanza ya msimu kwa mkopo klabu ya Valencia ya Uhispania. (Guardian)
Winga wa zamani wa klabu ya Manchester United Nani, 32, ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Sporting Lisbon, anatazamiwa kujiunga na ligi ya soka Marekani, MLS. (beIN Sport)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Januari 31, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2019 10:05:00 AM
Rating: