'Aliyefufuka' wakati wa mazishi yake afariki tena baada ya miezi miwili
Hirpha Negero |
Mawanaume mmoja aliyedaiwa kufariki miezi miwili iliyopita na kudaiwa kufufuka wakati wa mazishi yake, amefariki dunia.
- Soma na hii - Msiba wageuka kuwa sherehe baada ya marehemu kufufuka
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Hirpha Negero, raia wa Ethiopia alithibitishwa kufariki mwezi Novemba ambapo aliwekwa ndani ya jeneza kwa saa tano, lakini wakati wa mazishi yake wanavijiji walisikia akigonga jeneza.
Bw.Hirpha alisimulia BBC kwamba, "wakati huo nilisikia mtu akilia. Nilijihisi kuishiwa na pumzi ndipo nikajaribu kujitoa katika hali hiyo. Nilikua mnyonge , hata sikuweza kuzungumza. Hapakua na mtu yeyote karibu".
Katika simulizi yake baada ya tukio hilo, Bw.Hirpha alisema kuwa aliona 'mahali pazuri sana wakati alipokua amepoteza fahamu, ambapo mwanamume aliyekua amevalia nguo nyeupe alimwambia ''rudi nyumbani''.
Mchimba kaburi Etana Kena anasema watu walishtushwa na tukio hilo na kukimbia wakiliacha jeneza, ilibidi ajifungulie mwenyewe.
Hata hivyo daktari, Birra Leggese amesema kuwa huenda Hirpha alipoteza fahamu vibaya sana "deep coma".
Mchimba kaburi wa awali alimzika tena Hirpha kwa mara ya pili siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kifo chake na kuongeza kwamba safari hii alikua anauhakika wa kuwa amefariki kutokana na kushuhudia jinsi alivyougua kwa muda mrefu.

Reviewed by Zero Degree
on
2/01/2019 07:50:00 PM
Rating: