Sipendi kumuona Mbappe akibeba majukumu ya Neymar
Thomas Tuchel hataki kuona Kylian Mbappe akirundikiwa majakumu wakati huu ambapo Neymar akiuguza majeraha yake kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United kwenye hatua ya 16 bora.
Neymar amekuwa nje ya kikosi cha PSG tangu mchezo wao dhidi ya Strasbourg na anaweza kuwa nje hadi mwezi April. Mbappe na Neymar wamekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu hadi sasa wakiwa na Mabingwa hao wa Ufaransa hadi hivi sasa.
Kukosekana uwanjani kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu ya Barcelona inawezakuwa pigo kubwa, huku Tuchel akiwa na malengo ya kuelekeza nguvu zake kwenye Ligu ya Mabingwa na matumaini ya kuitwaa taji hilo katika msimu wake wa kwanza akiwa na vigogo hao.
Mbappe alitakiwa kubeba majukumu hayo lakini Tuchel anasistiza kwamba angependelea kuona Mfaransa huyo anacheza katika ari yake ya kawaida.
Kwa mujibu wa taarifa ya DailyMail, Tuchel alisema: “Huwa napendelea kumuona Kylian akicheza kama mmaliziaji – pale anapokuwa mtu wa mwisho dhidi ya wapinzani wetu.
“Huwa ni mtu hatari sana kwasababu ya kasi na njaa yake ya kupachika mabao.
“Sitaki kuona akibeba majukumu ya Neymar kutoa 'assist' na kumiliki mpira katika hatua za mwisho kutoka lango la maadui.
“Tuna wachezaji ambao wanaweza kufanya hivyo – wachezaji ambao wanaweza kumsapoti Kylian na Edi [Cavani] na kuwapa pasi nzuri za mwisho.
“Washambuliaji wote wanatakiwa kuwa wamaliziaji, hilo ndilo jambo la msingi.”
“Sitaki kuona akibeba majukumu ya Neymar kutoa 'assist' na kumiliki mpira katika hatua za mwisho kutoka lango la maadui.
“Tuna wachezaji ambao wanaweza kufanya hivyo – wachezaji ambao wanaweza kumsapoti Kylian na Edi [Cavani] na kuwapa pasi nzuri za mwisho.
“Washambuliaji wote wanatakiwa kuwa wamaliziaji, hilo ndilo jambo la msingi.”
Sipendi kumuona Mbappe akibeba majukumu ya Neymar
Reviewed by Zero Degree
on
2/07/2019 07:50:00 PM
Rating: