Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Februari 10, 2019
Manchester United wamewasiliana na wawakilishi wa Tanguy Ndombele kuhusu uhamisho wa kiungo huyo wa kati wa Lyon . (Le 10 Sport)
Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anasisitiza kulipwa mashahara wa £350,000 kwa wiki ambazo zitamfanya kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi nyuma ya Alexis Sanchez anayelipwa £400,000 kwa wiki .
Manchester United na Arsenal watatuma maskauti wao katika mechi ya Jumapili ya debi la East Anglian ili kumchunguza beki wa Norwich anayedaiwa kugharimu £10m Ben Godfrey, 21, ambaye amevutia klabu kama vile Lyon na RB Leipzig.
Uamuzi wa Beki wa Ajax Matthijs De Ligt wa kujiunga na ajenti maarufu Mino Raiola unaweza kuharibu uhamisho wake katika ligi ya Uingereza ,huku ikiaminika nchini Uholanzi kwamba klabu za Uingereza hazipendelei kufanya kazi na ajenti huyo.. Manchester City, Manchester United, Liverpool, Arsenal, Chelsea na Tottenham zote zinamlenga kinda huyo mwenye umri wa miaka 19.
Everton huenda ikamchukua mkufunzi wa Leeds Marcelo Bielsa iwapo watamfuta kazi mkufunzi Marco Silva. (Mirror)
Barcelona inafikiria kuimarisha safu yao ya ulinzi ya kushoto na sasa wanamlenga beki wa Lyon Ferland Mendy, 23, Filipe Luis, 33, wa Atletico Madrid na kinda anayelengwa na Real Betis Junior Firpo, 22,. (Mundo Deportivo)
Tottenham inahofia kwamba mchezaji wanayemlenga kumsajili Adrien Rabiot, 23, kutoka Paris St-Germain huenda akanunuliwa na Liverpool au Barcelona.
Chelsea inamfuatilia mshambuliaji wa Everton Richarlison, 21, ambaye pia ananyatiwa na klabu za AC Milan, Paris St-Germain na Atletico Madrid. (Star)
Manchester United ina mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon 18 kwa dau la paundi milioni 50 (Express)
Manchester United ina mpango wa kumsajili beki wa kushoto wa Fulham Ryan Sessegnon 18 kwa dau la paundi milioni 50 (Express)
Barcelona inafikiria kuimarisha safu yao ya ulinzi ya kushoto na sasa wanamlenga beki wa Lyon Ferland Mendy, 23, Filipe Luis, 33, wa Atletico Madrid na kinda anayelengwa na Real Betis Junior Firpo, 22,. (Mundo Deportivo)
Douglas Costa |
Winga wa Juventus winger Douglas Costa, 28, ametoa ishara kuhusu hatma yake ya siku zijazo alipopenda ujumbe wa twitter unaomuhusisha na uhamisho wa Manchester United. (Sun)
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Borussia Monchengladbach Max Eberl anatumai kwamba klabu hiyo itaweza kumshawishi Thorgan Hazard ambaye amehusishwaa na uhamisho wa Liverpool, kutia kandarasi mpya. (Inside Futbol)

Manchester City imeharakisha usajili wa kipa Gavin Bazunu, unaomfanya kinda huyo mwenye umri wa 16 kuichezea timu yake ya wachezaji wake wasiozidi miaka 18 siku ya Jumamosi-. (Manchester Evening News)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Februari 10, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
2/10/2019 05:35:00 PM
Rating: