Nahitaji kufunga mabao mengi mechi za kimataifa
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Prince Dube amesema mabao yake mawili aliyofunga na 'asisti' moja kwenye mechi mbili za kirafiki dhidi ya TS Galaxy na Kaizer Chiefs zote za Afrika Kusini, yamemfanya kujiamini zaidi na kujitabiria kufunga mabao mengi kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuanza Agosti 16, mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dube amesema awali hakuwa vema kwani hakucheza soka kwa muda wa miezi sita, lakini michezo mitatu aliyocheza imemrudisha kwenye uwezo wake ule ambao alikuwa anauhitaji kuwa nao kabla ya mashindano kuanza.
Ingawa hakuonekana kucheza vema katika mechi ya kwanza Afrika Kusini dhidi ya FC Augsburg ya Ujerumani ambayo timu yake ilifungwa mabao 2-1, alipachika bao pekee katika mechi dhidi ya TS Galaxy na kufunga tena mechi dhidi ya Kaizer Chiefs na kutoa pasi iliyozaa bao kwa Clement Mzize, Yanga ikiivurumisha timu hiyo mabao 4-0.
"Nimefurahi sana kwa michezo mitatu ambayo tumecheza Afrika Kusini, imenisaidia sana, imenirudisha kwenye kiwango changu kile ninachokifahamu, nilikaa muda mrefu bila kucheza soka la kiushindani, nimecheza mechi na timu za nje ya nchi, unajua ukicheza mechi kubwa kama hizi ina maana unaweza kucheza na timu yoyote kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na ukafunga mabao, nadhani hii imenifungulia milango, nahitaji kufunga mabao mengi mechi za kimataifa na nahitaji kuisaidia Yanga kupata mafanikio," alisema Dube.

Aidha, aliwashukuru wanachama na mashabiki wa klabu hiyo ambao wamekuwa wakimtumia salamu nyingi za kumpongeza ambazo nazo zinampa morali wa kuzidi kufanya mazoezi kwa bidii kuweza kuisaidia timu yao hasa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo alisema hakuwa anapata nafasi ya kushiriki.
"Kwenye ligi hakuna anayeweza kuhoji uwezo wangu, lakini Ligi ya Mabingwa Afrika nina muda mrefu sana sijacheza, nataka nionyeshe uwezo wangu huko, nimekuja Yanga kwa sababu hiyo tu, hivyo wanachama na mashabiki wasiwe na wasiwasi na mimi, nikishirikiana na wenzangu hakuna kitakachoshindikana," alisema mchezaji huyo raia wa Zimbabwe.
Alisema kitu kingine ambacho amebahatika kukikuta Yanga ni kucheza na wachezaji wawili anaowakubali, Clatous Chama na Stephane Aziz Ki, ambao amesema watamsaidia sana kwenye kazi yake ya kupachika mabao.

"Nimefurahi sana kucheza na wachezaji hawa, ni wachezaji wakubwa, ninajifunza vitu vingi kutoka kwao, na mimi nipo nao ili kuongeza kitu kwenye timu, najiona kama nina bahati ya kupata nafasi ya kucheza na wachezaji kama hawa," alisema Dube.
Chanzo: Nipashe
Nahitaji kufunga mabao mengi mechi za kimataifa
Reviewed by Zero Degree
on
8/01/2024 05:38:00 PM
Rating: