Loading...

Alichojibu Griezmann baada ya kuenea kwa tetesi za yeye kutaka kutimkia Man U.


Moja ya majina ambayo yametajwa sana kuhusu kuhama club zao ni Antoine Griezmann ambae alihusishwa sana na story za kuhamia club ya Manchester united kwa sababu mbalimbali.

Muda muafaka ndio huu umewadia na kila mwandishi anataka neno kutoka Griezmann kama atahama club yake ya sasa ya Atletico. Sasa kwenye mkutano na waandishi wa habari Griezmann aliulizwa kuhusu future yake ambapo moja kwa moja walitaka kujua kwamba kama ataenda Manchester au club yoyote.


Jibu lake lilikuwa kama hivi,“Silipendi hilo swali, usiniulize tena swali hilo kuhusu future yangu kwasababu wachezaji kama Ronaldo, Messi na Bale hakuna mtu yoyote anayewauliza nini kitatokea hapo baadae kwenye maisha yao ya soka au wapi watacheza tena. Ndio maana nami sipendi kuulizwa hili swali, nina furaha hapa nilipo na furahia maisha yangu ndani ya Atletico na sitaki tena kuulizwa kuhusu future yangu”

Jibu hili pamoja na maneno ya Jose Mourinho yanadhihirisha kwamba safari ya Griezmann kwenda united haipo kwa sasa hivi au inaweza isitokee tena. Jose alisema hatasajili mchezaji yoyote wala kuuza mchezaji yoyote kipindi hiki cha usajili.

ZeroDegree.
Alichojibu Griezmann baada ya kuenea kwa tetesi za yeye kutaka kutimkia Man U. Alichojibu Griezmann baada ya kuenea kwa tetesi za yeye kutaka kutimkia Man U. Reviewed by Zero Degree on 1/04/2017 05:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.